Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema askari wa Tanzania akifariki dunia akiwa katika vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa (UN), familia yake hulipwa fidia ya dola 70,000 za Marekani (zaidi ya Sh150milioni).

Dk Mwinyi ametoa ufafanuzi huo leo Jumanne Mei 8, 2018 bungeni mjini Dodoma na kubainisha kuwa kiwango hicho si cha mwisho kwa malipo kwa kuwa Serikali pia hutoa fedha za fidia kwa familia husika.
 
Ametoa maelezo hayo wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi aliyetaka kujua ni lini Serikali itapeleka bungeni mabadiliko ya sheria inayosimamia malipo ya fidia kwa askari anayejeruhiwa au kupoteza maisha akilinda usalama ndani au nje ya nchi.

Waziri amesema malipo ya fidia kwa askari aliyefariki au kujeruhiwa akiwa anatekeleza majukumu yake ya ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa husimamiwa na umoja huo.
 
Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Frank Joseph amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani akishtakiwa kwa wizi wa mahindi.

Joseph ambaye tukio la kukamatwa kwake liliibua hisia na mijadala mitandaoni ikidaiwa alishindwa kutua mzigo aliodaiwa kuuiba, alisomewa shtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nabwike Mbaba. Mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 124/2018 akidaiwa kuiba mahindi debe moja yenye thamani ya Sh20,000. Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa.
 
Hakimu Nabwike aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 10 ili kupata maelezo ya mlalamikaji ambaye hakuwepo mahakamani.

Licha ya mahakama kumweleza mshtakiwa kuwa dhamana iko wazi na kumpa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh500,000, alishindwa kutimiza sharti hilo hivyo alipelekwa rumande. Tangu Mei 3, Joseph alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani Pwani akituhumiwa kuiba mahindi kwa mkazi wa Mlandizi.
 
Ni kawaida mitindo ya uvaaji wa kisasa kuwa na nguvu mpaka kuushinda ushauri wa wataalam wa afya na matokea yake kutofuatwa na wanamichezo.

Wapo baadhi ya wanamichezo hasa vijana wanaopenda waonekane wana miguu midogo na hivyo kujikuta wakivaa viatu vinavyowabana pasipo kujua kuwa uvaaji huo una madhara kiafya katika miguu.
 
Kuvaa viatu vya michezo vya kubana kiujumla huwa na matokeo hasi kwa afya ya miguu ikiwamo maumivu baada ya kumaliza kucheza au wakati wa kucheza.

Kutokana na maumbile ya kiasili ya miguu eneo la chini ya ungio la kifundo cha mguuu ndilo linaloathirika zaidi ikiwamo vidole vya miguuni hasa dole gumba.
 
Madhara mbalimbali ya kiafya huibuka kutokana na viatu hivyo kubana katika seheme za mguu ikiwamo kucha, vidole, misuli, ngozi, nyayo, maungio ya vidole, kisigino, mishipa ya damu na fahamu.

Mara nyingi viatu vya kubana vinaweza kuwa vyembamba au vifupi sana kuliko ile saizi halisi ya mvaaji na pia eneo la mbele kuwa na upana mdogo au kuchongoka sana.
 
Mgandamizo wa viatu vya kubana huweza kusababisha kucha kukua vibaya na kuchimba katika kitako cha kucha na kusababisha jeraha.

Baadaye jeraha hilo huvamiwa kirahisi na bakteria na kutengeneza uambukizi mkali wa kidole ambao husababisha maumivu makali, homa, kuvimba na kuleta usaha.
 
Back
Top Bottom