Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

My kind of a woman [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
View attachment 769978
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji28][emoji28][emoji3][emoji28][emoji38][emoji38]
 
6F162FFD-CB11-41FB-A203-E3684C392414.jpeg
 
Kuna neno zuri ambalo hubeba maana kubwa kwenye tasnia yoyote ama kwenye utendaji kazi wa taasisi yoyote ile unaitwa nyuma ya pazia.

Nyuma ya pazia ni kule ambako hatukutazami kutokana na uwepo wa pazia ambalo huchukua “attention” yetu ama hukamata fikra zetu. Sifa ya mwanadamu ni kutazama kwa makini vile ving’aavyo kuliko vile visivyokuwa na mwanga.
 
Kwenye tasnia ya habari sifa anapewa mtangazaji kuliko mzalishaji, kwenye tasnia ya uigizaji sifa za anayeigiza kuliko anayetayarisha na hata kwenye kilimo jembe hupata sifa kubwa kuliko mpini.

Ni bahati mbaya lakini hivi vyote lazima vitokee ili shughuli ikamilike, yule anayechafuka hasemwi kuliko aliyekuwa msafi na aliyekuwa nyuma hazungumzwi kama anayekuwa mbele akitazamika.
 
Kwenye soka haya ni maisha ya kawaida pia na maisha yaliyozoeleka kila kukicha. Katika dunia ya Cristiano Ronaldo huwezi kumzungumza Toni Kroos, dunia ya Lionel Messi huwezi kumtaja Andres Iniesta kwa heshima anayostahili na hata katika dunia ya Pogba na Lukaku ni wazi utashangaa De Gea anaonekana anatimiza wajibu wake.
 
Ni jambo la kawaida na lililozoeleka kwa sasa, hata mmea unaostawi huwa tunavutiwa kwa kiasi kikubwa na maua yake, matunda yake na muonekano wake kuliko kazi kubwa iliyofanywa na mizizi ama shina kuhakikisha kuwa mti ule unakuwa imara na upo mahala pake.
 
Huwezi kuizungumza dunia ya soka kwa sasa pasipo kumtaja Mohamed Salah, mshambuliaji hatari zaidi kwa sasa. Binadamu pekee ambaye kila anachokunywa kina ladha ya zabibu, kila anachoshika ni dhahabu na sauti yake akizungumza inakuwa na mvuto wa chombo cha muziki ambacho bado hakijagunduliwa duniani. Yupo katika dunia ya kifikra ambayo watu wengi waliisubiri, dunia ambayo itaongezeka katika dunia mbili za Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
 
Amefunga mabao mengi zaidi ya raia yoyote wa Afrika katika msimu mmoja wa klabu bingwa Ulaya, amefunga mabao mengi zaidi kwenye msimu mmoja wa Ligi Kuu ya England.

Ametwaa kila tuzo anayotaka kuipata kwa msimu huu wa ligi na mwaka 2018 haujawa mwaka wa Jeff Bezos kutangazwa kuwa tajiri namba moja duniani bali umekuwa wa Mohamed Salah kuwa mwanadamu anayejeruhi kila lango linalopita mbele yake.
 
Amejenga urafiki na nyavu kuliko ngedere alivyokuwa na urafiki na miti, mabao yanafuata mkondo wa Mohamed Salah kuliko maji yanayotiririka mtoni kwenda baharini. Hakuna mwanadamu anayefanya maajabu ambayo hayakutegemewa kama Mohamed Salah kwa sasa, amegusa kila nyoyo na ameipa faraja ndani ya Anfield na mpaka kuitwa mfalme kwao Misri.
 
Back
Top Bottom