Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_20180508-071146.jpg
 
Lakini huyu anabaki kuwa kioo cha televisheni na hakuna anayetazama uchogo uliojificha, anabaki kuwa eneo limulikalo mbele kwenye kurunzi na hakuna anayejali betri zimekaa wapi. Anayo makali ya upanga kukata kilichokuwa mbele yake na wakati mwingine kuwa shoka anapokutana na vitu vigumu zaidi lakini hakuna anayejali mpini upo wapi. Anafanya madhara makubwa lakini kuna mwanaume ambaye ni muhimu zaidi ili nyumba anayoishi Mohamed Salah inayoitwa Liverpool iwe salama na inayokalika.
 
Huyu ndiye binadamu anayeamuru nguvu inayoweza kutumika siku hiyo kwenye kikosi cha Liverpool, anaamua kasi ya kukimbia ndani ya uwanja na anaamua kama iwe siku ya kivivu. Yeye ndio jiko ambalo linatoa pishi la Liverpool linaloitwa “Geggenpressing” mfumo maarufu unaotumika na Liverpool katika kuizingira timu pinzani ili kupokonya mipira kwa haraka. Anaitwa Roberto Firmino, Mbrazil anayefanana na wenzake katika kupenda starehe lakini akitofautiana nao katika uchapakazi.
 
Kwenye macho ya Brendan Rodgers, Firmino alikuwa namba 10 ambaye asingeweza kutulia kwenye mfumo wake kwa sababu eneo hilo alitaka mbwembwe za akina Coutinho na Lallana zaidi.

Bahati mbaya matokeo mabaya ya Liverpool kwa wakati huo yakasababisha Firmino awe muhanga wa kutumiwa kwenye nafasi tofauti zaidi na kila mtu akaona hii ilikuwa hasara nyingine mpaka alipofika Jurgen Klopp.
 
Back
Top Bottom