Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kweli kabisa. Wengi wanasema wanataman kuona soka likiendelea ila wakat huo huo hawataki uwekezaj wa muda mrefu na umilik halali mikonon mwa mtu mmoja. Cheki mazembe ipo mbali sababu ina boss mmoja mwenye saut moja inayosikilizwa na wote
Hapa Watu kumpa timu Manji hawataki sababu watakosa upigaji. Ikiwa vile wapigaji wengi. Tutaenda ado ado mpaka mwisho wa dunia.
Tanzania mpira upo tatizo wapigaji wengi.
 
Yanga ipo mtegoni mwa Simba

MUUNGWANA BLOG / 47 minutes ago



Kikosi cha Mabingwa wa soka nchini Yanga, kimeondoka jijini Dar es Salaam mchana huu kuelekea jijini Mbeya, tayari kwa mchezo wa Ligi kuu kesho dhidi ya Tanzania Prison huku ikiwa kwenye mtego wa ubingwa wa Simba.

Yanga imewasili jana ikitokea nchini Algeria ilikocheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger lakini imeunganisha leo kuwahi mchezo wake huo wa kesho ambao msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema wanauchukulia kwa umuhimu wake.

Yanga inakwenda Mbeya ikiwa kwenye mtego wa kutoa ubingwa kwa Simba endapo itatoa sare au kufungwa kwenye mchezo huo itakuwa imevua rasmi taji la ligi kuu baada ya kudumu nalo kwa misimu mitatu mfululizo.

Simba kwasasa inahitaji alama moja tu kuweza kuwa bingwa msimu huu hivyo inaweza isisubiri mchezo wake wa jumamosi na Singida United ili ianze kusherehekea ubingwa bali inaweza kufanya hivyo kesho endapo Yanga itakosa ushindi.

Mchezo huo wa kesho utapigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini humo. Yanga kwasasa ina alama 48 kwenye mechi 24 huku Simba ikiwa na alama 66 kwenye mechi 27.
 
Korea Kaskazini yawaacha huru raia watatu wa Marekani iliokuwa imewashikilia - Trump

MUUNGWANA BLOG / 48 minutes ago



Rais wa Marekani Donald Trump katika ukurasa wake wa Twitter asema kuwa Korea Kaskazini yawaacha huru raia watatu wa Maarekani iliokuwa imewashikilia.
 
Abdi Banda atwaa tuzo ya mchezaji bora

MUUNGWANA BLOG / 49 minutes ago



BEKI Mtanzania, Abdi Banda, anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Baroka, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili na Mei 2018 kwa upande wa klabu hiyo.

Mchezaji huyo ameisaidia timu yake kufunga mabao mawili na kuiwezesha kwenda sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ligi uliopigwa Aprili 28 dhidi ya Bloem Celtic katika Uwanja wake wa nyumbani,
Banda amekabidhiwa mpungwa wa rand 5000.00 kama ambavyo klabu hiyo hutoa kiasi cha fedha kwa kila mchezaji bora ndani ya mwezi.
Baroka FC imekshika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 34.
 
Back
Top Bottom