Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipa wa Ngorongoro Heroes arejeshwa kwenye kambi

MUUNGWANA BLOG / 49 minutes ago



Rais wa shirikisho la soka nchini (TFF) Wallece Karia amesema mlinda mlango wa Yanga na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes Ramadhani Kabwili amesharejea kwenye kambi ya timu hiyo.

Ramadhani Kabwili ameungana na wachezaji wenzake kambini baada ya utata kati ya klabu yake ya Yanga na kocha Ammy Ninje kumalizwa na Rais Karia hivyo sasa mambo yapo kama kawaida.

''Kabwili ameshajiunga na wenzie kambini na kilichotokea mpaka Kabwili kwenda nchini Algeria kuitumikia timu yake ya Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya U.S.M Alger ni kutokuwa na mawasiliano mazuri kati ya uongozi wa TFF na uongozi wa Klabu ya Yanga'', amesema.

Awali kocha wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje alimwondoa Kabwili kikosini na kumwita mlinda mlango wa Peter Doto Mashauri wa Black Sailor ya Zanzibar kiziba nafasi yake.

Ngorongoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Mali U20 Jumapili Mei 13, 2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20.
 
Tanzania yafungua ubalozi wake Israel

MUUNGWANA BLOG / 49 minutes ago



Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.

Afisi hizo za kibalozi zinapatikana katika mji wa Tel Aviv.

Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alikuwa amemualika Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi nchini Tanzania badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.

Waziri Mahiga, akizindua ubalozi huo Jumanne, alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania.

Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja hadi leo.

Sherehe za ufunguzi wa ubalozi huo zilihudhuriwa na Waziri wa Sheria wa Israel Ayelet Shaked.

Dkt Mahiga alisema Israel ni nchi ya kupigiwa mfano kwa sababu licha ya changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake bado nchi hiyo imepiiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo cha umwagiliaji.

Aidha, imepiga hatua katika sekta ya viwanda, matibabu, teknolojia ya habari na mawasiliano, ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na masuala ya nishati ikiwemo nishati ya kutumia joto ardhi.

Ufunguzi wa ubalozi huo ni muendelezo wa juhudi za kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili ambazo zilitiwa nguvu na ziara ya mawaziri wawili wa Israel nchini Tanzania mwezi Machi.

Waziri wa Ulinzi Avigdor Liberman alizuru Tanzania tarehe 20 hadi 22 Machi 2018 naye mwenzake wa Sheria Ayelet Shaked akafanya ziara ya kukazi tarehe 23 na 24 Aprili 2018.

Katika mkutano na Bw Lieberman ikulu ya Dar es Salaam, Rais Magufuli alikuwa ametaka makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama, mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanze mara moja.

"Tanzania na Israel ni marafiki wa miaka mingi, nataka kuona urafiki wetu unakuwa zaidi, nawakaribisha wawekezaji kutoka Israel kuja kuwekeza katika kilimo, madini na gesi na pia kuwepo ndege za moja kwa moja kutoka Israel hadi Dar es Salaam na Kilimanjaro ili kukuza utalii" alisema Dkt Magufuli.

Katika ziara hizo masuala mbalimbali yaliafikiwa ikwemo Israel kuisaidia Tanzania kuanzisha chombo cha kutoa msaada wa kisheria kwa wasiojiweza ambacho kwa upande wa Israel kimeshaanzishwa na kina mafanikio makubwa.

Dkt Mahiga, akuzungumza Jumanne aliwakaribisha Waisrael kuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii kwa kuwa Tanzania ina vivutio lukuki vya utalii.

Alisema zaidi ya watalii 50,000 hufika Tanzania kila mwaka lakini hawatoshi kutokana na wingi wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.


 
Aliyeolewa mara 11 auawa na Al - Shabab

MUUNGWANA BLOG / 50 minutes ago



Mwanamke mmoja amepigwa na mawe mpaka kifo nchini Somalia baada ya mahakama moja inayoendeshwa na kundi la wanamgambo wa kiislamu, al-Shabab kumkuta na hatia ya kuolewa na wanaume wengi.

Shukri Abdullahi Warsame alishutumiwa kuolewa mara 11 bila kutalikiwa na waume zake waliopita.

Sehemu ya kiwiliwili chake kilifukiwa ardhini kichwa kikiachwa juu kisha akapigwa mawe na wanamgambo mjini Sablale mpaka umauti.

Mwaka 2014,wapiganaji wa al-Shabab walimpiga mwanamke mmoja na mawe baada ya kumshutumu kuolewa na wanaume wanne kwa siri, wilaya ya Barawe nchini humo.
 
Makonda awaonya Wakandarasi Dar

MUUNGWANA BLOG / 50 minutes ago




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaonya wakandarasi wenye tabia ya kutengeneza Barabara za chini ya kiwango na kuharibika ndani ya muda mfupi jambo linalosababisha hasara kwa serikali na usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.

Makonda ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya utiaji wa saini kwa Mikataba Nane ya mradi wa matengenezo ya Barabara, Mifereji ya Maji na Culvets inayotekelezwa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA yenye tahamani ya zaidi ya Billion 5.8 ambapo amewataka TARURA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hizo.

Aidha Makonda amezitaja Barabara zitakazojengwa kupitika mradi huo kuwa ni pamoja na Tegeta Nyuki, Msasani, Magomeni Makuti,Migombani, Kimara baruti, Kibanda cha Mkaa, Sheikh Bofu, Kwa Komba, Msigani, Sea clif na Mwananyamala Kisiwani




Hata hivyo Makonda ametoa wiki mbili kwa TARURA kuhakikisha wakandarasi waliojenga barabara chini ya kiwango zinajengwa upya kwa gharama ya mkandarasi ikiwemo barabara ya Mabatini ambapo barabara hizo zitakuwa na mifereji ya maji, sehemu za watembea kwa miguu na Taa za Barabarani.

Pamoja na hayo Makonda amesema katika uongozi wake hawezi kufumbia macho matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi hivyo atahakikisha anasimama kidete kuhakikisha Dar es salaam inakuwa na barabara zenye ubora.

Sanajari na hayo Makonda ametaka uwepo wa ushirikiano wa kikazi baina ya TARURA, TANROAD, TANESCO, DAWASCO na TTCL ilikupunguza ucheleweshaji wa miradi na ujenzi usiofuata taratibu unaopelekea uharibifu wa miundombinu.
 
VIDEO: Mbunge CHADEMA nusura amwage chozi Bungeni

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago




Mbunge wa Jimbo la Mlimba Morogoro kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Suzan Kiwanga amewasha moto bungeni ambapo amesema changamoto ya maji jimboni kwake imekuwa kero kwa wananchi.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KUSUBSCRIBE



 
VIDEO: ''Tuuze ndege 2 tutatue tatizo la maji, CCM hamna Waziri mzigo'' Mbunge Cuf

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago




"Wananchi wa Kilwa wananunu maji ndoo shilingi 1000 kupeleka hospitali ya Wilaya ambayo haina maji, alafu nyinyi mnanunua ndege maskini ni bora tuuze ndege mbili tutatue tatizo la maji" Mbunge wa Kilwa Kusini Selemani Bungara marufu kwa jina la Bwege.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE



 
Mahudhurio hafifu ya wanafunzi wa kike yapatiwa ufumbuzi

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Katika kuonesha kuwa wanaunga mkono na kuthamini suala la elimu kwa watoto wa kike, Watumishi wanawake wa Manispaa ya Ilala wameanzisha kampeni waliyoipa jina la 'Binti makini mwamvuli wangu stara' yenye lengo la kujenga vyoo kwenye shule zilizopo kwenye manispaa hiyo.


Kupitia tafiti mbalimbali zinazofanyika kuhusiana na sababu zinazochangia mahudhurio hafifu ya watoto wa kike mashuleni hususani wale wa darasa la saba zinaeleza kuwa vyoo hafifu na visivyofaa kwa watoto wa kike kipindi cha hedhi ndiyo sababu kubwa ya mahudhurio hayo.


Hivyo kwa kutambua changamoto hiyo inayowakabili watoto wa kike, Watumishi hao wamesema wameanzisha kampeni ya kujenga vyoo maalumu ambavyo vitawawezesha kushiriki kikamilifu masomo yao badala ya kubakia nyumbani wakati wa hedhi hali inayoathiri mtiririko wa maudhui ya yale yanayofundishwa shuleni.


" Uzinduzi wa kampeni hii unatarajiwa kufanyika Mei 11, mwaka huu katika ukumbi wa Lamada na mgeni rasmi atakua Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, tunashukuru namna ambavyo watumishi wa manispaa walivyojitoa kuhakikisha kuwa tunafanikisha azma yetu hii ya kuwasaidia watoto hawa ambao ni watoto wetu, wadogo zetu pia.


" Kampeni ya ujenzi wa choo kwa ajili ya mtoto wa kike itaanzia kwenye shule 120 za msingi zilizopo kwenye manispaa ya Ilala na kuendelea katika shule za sekondari, tunaamini lengo letu la kuondoa zile siku nne ambazo takwimu zinasema watoto hawa ndio wanakua wanazipoteza ndani ya mwezi mmoja sasa zitaondoka kwa kuwa changamoto imetatulika," amesema Mratibu wa Kampeni hiyo Tabu Shaibu.


Choo kitakachojengwa kitakuwa na matundu 10, maji ya kutosha, masinki ya kunawia mikono, kabati la kuhifadhi taulo za kik, kioo na sehemu ya kuchomea taka. Gharama za ujenzi zinakadiriwa kufikia sh 20,000,000.
 
Wabunge watano wajiuzulu kwa kuwa na uraia wa nchi mbili

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Wanasiasa watano nchini Australia wamelazimika kujiuzulu kutokana na kugundulika kuwa na uraia wa nchi mbili kipindi ambacho walichanguliwa kushika nafasi hizo.

Mwaka jana, wabunge 10 nchini humo pia walivuliwa ubunge kutokana na kuwa na uraia wa nchi mbili tofauti na katiba inavyohitaji kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Suala la uraia wa nchi mbili linatajwa kuyumbisha Bunge na serikali ya Australia kwa ujumla tangu mwezi July, 2017 na limewahi kuhatarisha baraza la mawaziri.
 
[HASHTAG]#naona[/HASHTAG] "kula like " mara pata "Like "

Emb fanyen kutest Mitambo hapo na mimi nitest kwako..
 
Serikali yawahakikishia jambo hili wananchi wa Kigamboni

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso imewahakikishia wananchi wa Kigamboni wanapata Maji Safi na salama na yanayowatosheleza.

Aweso ameyasema hayo leo Bungeni, wakati akijibu la Mbunge aliyehoji Je ni lini serikali itawapatia Maji Safi na Salama wananchi wa Kigamboni?

“Mimi kama Naibu Waziri nilipata kibali cha kutembea mkoa wa Dar es salaam na moja ya maeneo niliyofanya ziara ni Wilaya ya Kigamboni, Temeke na maeneo mengine ni kweli zipo changamoto katika suala zima la maji hususani pembezoni mwa Dar es salaam,“ amesema Aweso.

“Sisi kama Wizara ya Maji tumechimba pale Mpera na Kimbiji visima 20 katika kuhakikisha tunatatua tatizo hili la maji. Sisi kama Wizara ya Maji na kwakuwa si Wizara ya ukame tupo tayari kuhakikisha wananchi wa Kigamoni wanapata Maji safi na salama na yanayo watosheleza.“
 
Hatima ya Antonio Conte kujulikana mwisho wa msimu

MUUNGWANA BLOG / 4 hours ago




Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa atafanya maamuzi ya aidha kuondoka au kusalia ndani ya kikosi hicho utakapofika mwishoni mwa msimu.

The Blues watacheza mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Manchester United Mei 19 uwanja wa Wembley ikiwa ni ishara kuwa ndiyo mechi yake ya mwisho Conte akiwa kocha wa timu hiyo.

Alipoulizwa swali na waandishi wa habari kama angeendelea kusalia Stamford Bridge msimu ujao mara baada ya mchezo wake wa mwisho wa ligi dhidi ya Huddersfield amesema kuwa bado hajafanya maamuzi mpaka atakapo hakikisha amemaliza msimu.

Mpaka sasa nimechanganyikiwa na uwepo wangu hapa, kufanya kazi vizuri na wachezaji pamoja na mashabiki. Kazi yetu siyo rahisi na wala siyo nyepesi hata kidogo lakini kwakuwa bado nipo ninachofikiria ni hapa nilipo.

Zimesalia wiki mbili pekee msimu huu kumalizika hivyo mtafahamu kama kutakuwa na mabadiliko ama laa.

Chelsea itashuka dimbani kuikabili Huddersfield huku ikiwa inahaha kuhakikisha inapata nafasi ndani ya ‘top four’ kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ili kujihakikishia kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
 
MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

MATUKIO @ MICHUZI BLOG / 58 minutes ago





Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah.



Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae kulia ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).



Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela.



Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.



Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.


Dar es Salaam, 09 Mei 2018. Mashindano maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia kuwavutia mashabiki wengi wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote wa mbio hizo.


Katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’ ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo.


Baada ya majadiliano ya kina na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es salaam, Oysterbay iliamua kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa yake mpya ya “The Rotary Goat Races,” mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam, yakitegemea kutumia rasilimali za mwanzo zilizotumiwa katika michuano iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni la kiburudani na kifamilia na mapato yake yataelekezwa kwenye miradi ya hisani.


Tofauti na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.


"Kimataifa, Rotary na vilabu vyake wana sifa ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa kupitia wanachama wake wa kujitolea, wakielekeza karibia asilimia mia ya fedha zote za miradi kwa walengwa”, alisema raisi wa sasa wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay, Anne Saels. “Tunaamini kwamba kupitia miradi ya elimu iliyopangwa tunaweza kuleta tofauti kubwa kwenye maisha ya watu katika jamii na tunafuraha kuwa mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary yatakuwa na jukumu muhimu katika kukamilisha hili”.


Mwenyekiti wa bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah anaamini kuwa mashindano hayo kwa mwaka huu hayatawaangusha mashabiki. “Kwa motto ya ‘Wakanda Goat Are You’,tukikumbuka muvi iliyofanya vizuri kwa mwaka huu ya ‘Black Panther’, tunatumai kuwavutia mashabiki wapya na wadau wa mbio za mbuzi vilevile”,aliongea mwenyekiti huyo.


Kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita, mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yamefanikiwa kuvutia wadhamini wakuu kama vile Toyota, Swiss International Airlines na Coca Cola. Tunashukuru kwa imani ya wadhamini wetu katika shirika letu na tunaamini kuwa mashindano ya mbio za mbuzi ya Rotary kwa mwaka 2018 yatakuwa ya burudani kwa kila mmoja”.


Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay ilianzishwa mwaka 2009 na hadi sasa ina wanachama 70. Ni klabu kubwa zaidi miongoni mwa Klabu za Rotary nane jijini Dar es Salaam na inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Afya ya Jamii ambao huandaa makambi ya matibabu ya mara mbili kwa mwaka kwa vijijini na mijini, mradi wa Vijana Poa wa kusaidia vijana wa chuo kikuu kupata kazi , mbio za Rotary Dar, kusaidia kazi za hospitali ya CCBRT na Rotary Mission Green ambazo ni jitihada za kwenye wilaya za kupanda miti. Zaidi ya hayo, Klabu ya Rotary ya Oysterbay kwa sasa inajenga Rotary Community Corps, mradi ambao umejikita katika kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wanufaika katika jamii.

Visit website
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…