Mtaalamu mwingine, Chantelle Crabb alisema, uvaaji wa sidiria ambayo haiendani na ukubwa wa maziwa ya mwanamke kunaweza kusababisha maumivu ya matiti, aibu na uharibifu wa matiti. Lakini alifafanua zaidi kwamba, uvaaji vibaya wa sidiria unaweza kupelekea matiti ya mwanamke kulegea/kulala.
Mbali na hayo, madhara mengine ni pamoja na maumivu ya mgogo kwani mwenye maziwa makuba akivaa sidiria ndogo hulazimika kuinama anapopita katika eneo lenye mwinuko.
Kuhusu kupata saratani ya matiti/titi, Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Cyrill Massawe alisema kuwa, wanawake wanapaswa kuvaa sidiria zinazoendana nao ili wawe huru, huku akisema hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuvaa sidiria ndogo na saratani ya matiti.