Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zidane afunguka

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Kocha wa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid Zinedine Zidane amesema nyota wa timu hiyo Cristiano Ronaldo atakuwa imara kwa asilimia 150 kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Mei 26.

Akiongea leo mbele ya wanahabari kuelekea mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya Sevilla, Zidane amesema, Ronaldo ataukosa mchezo huo kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu lakini atakuwa vizuri kwenye mechi ya fainali.

''Hatutakuwa na Ronaldo ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Barcelona, yupo kwenye matibabu na anaendelea vizuri na tunauhakika kwa asilimia 150 atakuwepo kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Liverpool'', amesema.

Ronaldo alitolewa kwenye mechi ya El Clasco baada ya dakika 45 za kwanza kutokana na kuumia wakati akifunga bao la kusawazisha kwa Real Madrid. Zidane amesema wachezaji Dani Carvajal na Isco pia wanatarajia kurejea mpaka wakati wa mchezo huo.

Reala Madrid inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, kesho itacheza na Sevilla inayoshika nafasi ya 8 kwenye msimamo huo. La Liga imebakiza mechi tatu kumalizika huku ikiwa tayari Barcelona wameshatwa ubingwa.


 
Mgodi wa Almasi wagunduliwa katika gereza

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Mgodi wa madini ya Almasi wagunduliwa katika gereza moja Kaskazin-Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mamlaka husika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefunga gereza hilo na kuwaamisha wafungwa baada ya kupata taarifa mwishoni mwa wiki iliopita kuwa wafungwa walikuwa wakichimba almasi kwa muda wa wiki kadhaa katika gereza hilo.

Mmoja miongoni mwa viongozi katika eneo la Osio Tshopo mjini Kisangani, almasi imegunduliwa katika gereza la Osio Kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wafungwa katika gereza hilo wamethibitisha taarifa hiyo na kufahamisha walikuwa wakishirikiana na baadhi ya viongozi katika gereza hilo.
 
Tume maalumu kushiriki katika ufunguzi wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Tume maalumu kutoka Marekani yatarajiwa kuwasili mjini Yerusalemu kushiriki katika hafla ya ufunguzi wa ubalozi wa Marekani mjini humo.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa Marekani itahamisha ubalozi wake uliopo Tel Aviv na kuhamia mjini Yerusalemu. -Uamuzi huo ulipelekea maandamano na mataifa kama Uturuki kuitisha mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa kukemea uamuzi huo.

Umoja wa M ataifa ulifanya mkutano ambao ulikemea uamuzi wa Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump hatushiriki katika ufunguzi wa ubalozi huo Yerusalemu.

Taarifa kuhusu tume hiyo kujielekeza Yerusalemu kushiriki katika ufunguzi wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu ilitolewa na ikulu ya WHite House Jumatatu. John Sullivan ndie atakae ongoza tume hiyo kutoka Marekani.

Ufunguzi wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu unatarajiwa kufanyika ifikapo Mei 14.

Watakaoshiriki katika ufunguzi huo ni balozi wa Marekani Israel Tume kutoka Marekani David Friedman, Steven Mnushin, mshauri na mkwe wa Trump Jared Kushner, Ivanka Trump na mpatanishi wa Trump Jason Greenblatt.
 
Ozil atupiwa lawama na Wachezaji wa Arsenal

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Mesut Ozil ni moja kati ya majina makubwa katika Ligi Kuu England kwa sasa hususani katika club ya Arsenal kwani yeye ndio mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi ya wachezaji wote wa Arsenal.

Jina la kiungo wa Ujerumani linazidi kuchukua headlines kufuatia stori zinazoripotiwa katika mitandao kuwa Mesut Ozil amekuwa na tabia ambayo sio nzuri licha ya kuwa ndio mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ya wachezaji wote wa Arsenal.

Wachezaji wa Arsenal wanadaiwa kuhoji tabia ya Ozil na kudai kuwa hajitoi kwa kiasi kikubwa katika timu ukizingatia amekosekana katika game 5 za Arsenal zilizopita na sasa inaripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu hadi Kombe la Dunia litakapoanza.

Inaripotiwa kuwa Ozil anayelipwa mshahara wa pound 350000 kwa wiki licha ya kuwa anatajwa kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi, wenzake wanaona tabia ya Ozil kudai kuwa na majeruhi ni kama tabia ya kuchagua mechi za kucheza kwani katika game 58 za Arsenal msimu huu Ozil ameanza katika game 25 pekee.

Kwa upande wa kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameonekana kutoa kauli za kumtetea “Mchezo wa mpira hauko hivyo na sio kama anachagua mechi bali ni majeruhi madaktari wameniambia kuwa ni hatari kumchezesha kwa sasa itakuwa ni hatari sana kujaribu kumtumia akiwa hayupo fiti”
 
Rais Trump ampongeza rais Putin

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Rais Donald Trump ametoa pongezi kwa rais wa Urusi Vladmir Putin baada ya kuapishwa kwake.

Putin ameapishwa kama rais wa Urusi kwa muhula wa nne.

Msemaji wa ikulu ya White House Sara Sanders amesema kuwa Trump ana imani Urusi na Marekani zitaendelea kuwa na uhusiano mzuri.

Putin, ambaye alipata asilimia 76.69 ya kura katika uchaguzi wa Machi, atatumikia nafasi hiyo hadi 2024.

Vilevile Trump alimpigia simu ya pongezi Putin baada ya kushinda uchaguzi mkuu mwezi Machi.
 
Mwakyembe: Tutabaki wasindikizaji tu

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameutaka uongozi wa Baraza la Michezo nchini (BMT) kufuata yale yote yanayotakiwa katika utendaji kazi wao ikiwemo kutekeleza kazi za nyongeza alizowapa ili kuhakikisha michezo inakuwa nchini.

Waziri Mwakyembe amesema hayo hii leo Mei 08, 2018 wakati wa kuzindua Baraza la 14 la michezo ambapo amelitaka Baraza hilo kuhakikisha wanakuwa na mda wa kukutana na wadau wa michezo ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wilaya na mikoa ili kuhakikisha vyama pia vinakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu michezo.

"Kutokana na hali halisi ya michezo hapa nchini kwetu, nimeamua kutoa kazi za nyongeza kwa Baraza ambapo kazi hizo zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini, kubwa zaidi ya yote ni kulitaka Baraza kuhakikisha vyama vinaheshimu katika zao kwa kufanya uchaguzi ndani ya mda waliopanga ili kuweza kutoa nafasi kwa wanachama wao kuweza kusapoti mchezo huo na kuuendeleza", amesema Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Waziri Mwakyembe ameendelea kwa kusema "hatuna budi kuwekeza kwa watoto ambao ndio watakaoweza kuinua michezo hapa nchini na bila hivyo daima tutabaki wasindikizaji kwa kila mchezo na tutakuwa tukilalamika tu bila kujua tunatakiwa kurekebisha wapi".

Kwa upande mwingine, Waziri Mwakyembe amesema ipo haja ya kuwekeza kwenye miundombinu ya kimichezo hapa nchini ili kuhakikisha watoto pindi wawapo katika viwanja vya michezo wanakuwa katika mazingira yaliyokuwa bora ya kimichezo.
 
TFF yaziagiza klabu za Yanga na Coastal Union kufanya uchaguzi

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Shirikisho la Soka nchini TFF limeziagiza klabu za Yanga na Coastal Union kufanya uchaguzi ili kuziba nafasi za viongozi wao walioachia ngazi.

Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Rvocatus Kuuli, imeeleza kuzitaka timu hizo kufanya uchaguzi huo ili kujana nafasi ambazo zipo wazi.

Hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji aliachia ngazi kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa madai ya kuwa alihitaji kupumzika.

Mbali na Yanga pamoja na Coastal Union, AFC Arusha nayo inatakiwa kuungana na timu hizo tajwa hapo juu kufanya uchaguzi huo.


 
Hofu ya Marekani kujitoa katika mkataba wa Nyuklia

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Rais wa Iran Hassan Rouhani ameonya uwezekano wa kutokea matatizo endapo rais wa Marekani Donald Trump atafanya uamuzi wa kuitoa Marekani katika makubaliano ya kinyuklia na mataifa makubwa duniani.

Bila kumtaja moja kwa moja Rais Trump, matamshi ya Rouhani katika mkutano wa wazalishaji wa mafuta uliofanyika mjini Tehran yanawakilisha matamshi ya kwanza rasmi ya Iran kuhusiana na ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba alitarajiwa kutoa tamko kuhusu mustakabali wa Marekani katika makubaliano hayo

Rais Rouhani amesisitiza kwamba Iran inataka kufanya kazi pamoja na mataifa mengine duniani kuiweka dunia katika hali ya usalama.
Wakati hayo yakijiri Serikali ya Ujerumani imetilia mkazo nia yake ya kuendelea kuunga mkono mkataba wa nyuklia wa Iran, wakati ambapo hatma ya mkataba huo inafikia ukingoni.
Trump anatarajiwa kutangaza maamuzi ya kuendelea ama kujiondoa kwenye mkataba huo ifikapo Mei 12.
 
Jinsi Ya Kujenga Mafanikio Ukiwa Na Mtaji Wako

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Na siku ya leo tutakwenda kujibu moja ya swali ambalo tumekuwa tukiulizwa sana na wasomaji wetu kwamba ni jinsi gani mtu anavyoweza kujijengea mafanikio ukiwa na mtaji wake.

Nasi kwa kuwa hatufungamani na upande wowote tutakwenda kujibu swali hili pasipo kuona aibu, hii kwa sababu moja ya kati ya kauli mbiu yetu inayotuongoza katika kufanya kazi, ni kuwafanya watu wote pasipo kuangalia dini wala kabila wawe na fikra sahihi kila wakati ili waweze kufanikiwa.

Na ukweli ni kwamba moja kati ya maswali ambayo watu wengi wanayo ni pamoja na hili, hii ni kwa sababu watu wengi huwa wanasema hawajafanikiwa kwa sababu hawana mtaji, lakini mara baada ya kupata mtaji utakuta watu haohao wanakosa katika mtaji huo wafanye kitu gani, swali linakuja hivi hujawahi kukutana na mtu akakwambia ya kwamba nina mtaji wa shilingi laki mbili lakini sijui nifanye kitu gani?

Bila shaka umewahi kukutana aina hii ya watu na kama hujawahi kukutana nao basi yawezekana ukawa ni wewe. Najaribu kujiohoji kwa sauti kubwa hivi hapa tatizo huwa linakuwa ni nini, mtu asipo fanikiwa atakwambia tatizo ni mtaji ila mara baada ya kupata mtaji atakwambia hajui afanye nini katika mtaji alionao.

Kwa muktadha huo hapa utagundua ya kwamba tatizo ni mawazo, narudia tena tatizo la watu wengi kutofanikiwa aidha kwa kuwa na mtaji au kwa kutokuwa na mtaji tatizo huwa ni mawazo chanya ni nini mtu afanye ili aweze kufanikiwa.

Hivyo kitu cha msingi cha kuzingatia ili uweze kufanikiwa ukiwa na mataji wako ni kujua unataka nini katika maisha yako, hiki ndiyo kiwe kitu kikubwa cha kuzingatia kitakachokufanya wewe uweze kufanikiwa Zaidi.

Haijalishi ni kiasi gani ambacho kipo mkono mwako, kama lengo ni kuwa mfanyabiashara wa aina fulani ni vyema ukakaa chini na kutafakari kwa kina, tafakari kwa kina pasipo kuchoka. Na kutafakari huku kwa kina hakikisha anafanya uchanganuzi wa kutosha juu ya jambo unalitaka kulifanya.

Kwa mfano mkononi unayo laki tano kwa ajili ya mtaji fanya tathimini ya biashara ambayo unataka kuifanya, na tathimini hiyo hakikisha haimalizi mtaji wote kwa mara moja. Kama nilivyosema hapo awali kama una mtaji wa shilingi laki tano basi tathimini ya biashara yako iwe ni la shilingi laki nne. Kufanya hivi kutakusadia laki moja iliyobaki kuweza kutatua changamoto ndogondogo ambazo zitajitokeza katika biashara yako.

Hata hivyo katika biashara hiyo ambayo utakuwa umeanza kuifanya ni lazima uwe na daftari la mahesabu ya biashara yako, daftari hili utaandika mapato na matumizi katika biashara yako, kufanya hivi itakusaiadia kujua kama unapata faida au laah. Pia mali bila daftari hupoteaa bila habari.

Lakini jambo jingine katika mtaji ulionao hakikisha unaulinda kwa nguvu zote kama mboni ya jicho lako, kufanya hivi kutakutoa wewe katika orodha ya watu ambao huanzisha miradi au biashara kisha biashara hizo kufa.
 
Zitambue mbinu za mafanikio katika kilimo

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



1. Zalisha kwa wingi.
Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.

2. Tafuta masoko ya bidhaa kabla ya kuanza uzalishaji.
Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako. Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza wateja na wateja watakutengenezea biashara.

Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.

Unafuu wa bei

Ubora wa zao

Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa


Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa umejihakikishia soko la uhakika

3. Usilime kwa kuafata misimu.
Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara muda mwingine.

Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.


4. Epuka kufanya kilimo kwa mazoea

Tumia wataalamu wa kilimo

Tumia njia za kisasa za kilimo

Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia wataalamu)

Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri zaidi
 
Aise,, [emoji16] [emoji16] [emoji16]
Umefuraaahiii... Kumbuka hilo jina lako lina ashiria na wewe ni wa Mwakaleli japo haujawahi kufika kabisa(ningendako) huko...
Karibu kwetu, au kama vipi karibu Keko Mwanga/Magurumbasi,Msasani au Mabibo utajisikia upo unyakyusani[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Good morning brother[emoji120] [emoji120]
Enjoy the day
 
Mambo 7 yanayowaumiza wanaume kwenye mahusiano

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa.

Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.

Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye
kukimbiwa.

Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama.

Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa.

Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.

1. Chokochoko/Maneno Maneno
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. Kutoridhika
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.

Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. Kulinganisha
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’

Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. Kuwa Tegemezi
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.

Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. Kutokuwa Muelewa
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.

Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. Kujigamba/Maringo
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. Kuwa bize sana
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.
 
Chunga Sana Matumizi Haya Ya Pesa Ili Yasikupoteze

MUUNGWANA BLOG / 1 day ago



Kitu cha msingi unachotakiwa kuzingatia wakati unatumia pesa zako, ni ubora wa vile vitu ambavyo unakwenda kuvipata wakati unatumia pesa zako.

Kama unatumia pesa zako kwa vile vitu ambavyo viko bora wakati wote, basi pesa zako wakati wote ziko salama na zitakusadia kupiga hatua ya aina fulani.

Kama unatumia pesa zako kwa mambo ya hovyo hovyo basi hata kama kipato chako ni kikubwa kiasi gani, pesa hizo utakuwa unazipoteza tu bure na hakuna unachofaidi.

Wakati wote unatakiwa kuzingatia ni kwa namna gani unafanya matumizi yako kwa ubora, ikiwa unafanya matumizi yako kwa ubora utajiweka kwenye wakati bora pia.

Watu wengi wanajikuta wameishia na hawana kitu kwa sababu ya kufanya matumizi yasiyo ya msingi, bali wanafanya matumizi ya kuwabomoa.

Kila wakati chunga matumizi yako na hakikisha unajua pesa zako zinakwenda wapi kila siku iitwapo leo.

Kutumia zako hovyo, huko ni kujitakia majanga yaw ewe kuweza kuishia kwa baade. Tumia pesa zako kwa busara nazo pia zitakulinda.
 
Back
Top Bottom