Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BREAKING NEWS: Sugu na Katibu wa CHADEMA Masonga wameachiwa huru

MUUNGWANA BLOG / 45 minutes ago




Leo May 10, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya ambapo walikuwa wanatumikia kifungo cha miezi 5.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amethibitisha kuachiwa kwa Viongozi hao wawili na tayari Sugu ameshafika nyumbani kwake.

Wengine waliofika gerezani kumpokea ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani, Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda
 
Zijue Faida Na madhara ya Matumizi Ya Chumvi Kifua

MUUNGWANA BLOG / 8 hours ago




Bila shaka kila mmoja wetu anapenda sana kuitumia chumvi, na hii hutokea hasa pale anapokula chakula chenye uhitaji wa chumvi. Lakini Watu wengi wamekua wakiitumia chumvi kulingana na matakwa yao binafsi bila kujua bila kujua chumvi ina mahusiano yapi afya zao. Wengi hutumia kwa ajili ya kupata radha katika chakula anachokula.

Wengi wetu wanakula chumvi bila hata kujua kiwango gani cha chumvi hitachohitajika mwilini? Je wewe ni miongoni mwa watu hao? Kama jibu ni ndio nakusihi ufutane na Dr. Julius Kimaro katika Makala haya kwani ameeleza kwa kina zaidi. Ambapo Anasema:

CHUMVI
Kikemia chumvi ina madini ya sodium chloride ambayo huitajika sana mwilini. Na madini hayo husaidia kwa kiwango kikubwa katika mwili wa mwanadamu kama ambavyo nitaeleza hapo chini:

Faida za chumvi
Moja kati ya faida kubwa ya chumvi ni kuweka sawa kiwango cha maji mwilini (fluid balance) kinachoptaikana katika mwili wa mwanadamu.

Chumvi husaidia katika kuweka sawa mtiririko wa mapigo ya moyo (heart rhythm) pale inapotumika kwa usahihi.

Husaidia katika kutanuka na kusinyaa kwa misuli (contract and relax of muscles), ambapo misuli hiyo husaidia kwa kiwango kikubwa usafishaji wa damu na maji endapo itakuwa haijaithiriwa na kiwango cha chumvi kwa wingi.

Madhara ya chumvi.
Madhara makubwa yatokanayo na ulaji mbaya wa chumvi ni shinikizo la damu (blood pressure). Kwani ukweli usiopingika ni kwamba kuna mahusiano ya moja kwa moja ya utumiaji wa chumvi kwa wingi na na kupanda kwa presha.

Hata hivyo wataalamu wa afya wamebaini ya kwamba uwepo sodium ambayo ipo kwenye chumvi ndiyo chanzo kikubwa cha kuasababisha ugonjwa huo. Kwani tafiti zinaonesha ya kwamba binadamu akitumia chumvi kwa asilimia 40 ya uzito wake ana uwezo wa kupunguza kupata shinikizo la damu.

Nini kifanyike:
Muhumu kuzingatia kuwa kiwango salama cha chumvi kwa mtu mzima hutakiwa kula chumvi kiasi cha 500 milligram ambayo ni sawa na robo ya kijiko cha chai kwa siku ili kuweza kuepukana na matatizo yatokanayo na ulaji wa chumvi kwa wingi.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema, na usisiahau kumshirisha na mwingine ujumbe huu, ili kulinda kizazi hiki kwa kuepeka matumizi mabaya ya chumvi.
 
Ufugaji Bora Wa Sungura

MUUNGWANA BLOG / 12 hours ago





UTANGULIZI

Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu.


MABANDA

Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.


UFUGAJI WA NDANI

1. Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha

2. Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa

3. Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri

4. Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi

5. Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki.


UFUGAJI WA NJE

1. Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk

2. Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika

3. Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali

4. Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng’oa yote)


MAJI

Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku.


CHAKULA

Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates).


USAFI

Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura

mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto.


MENO

Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12.


MIGUU

Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana.


UBEBAJI

Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba.


DAWA

Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine

bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo.
 
Mnyika na Bulaya watolewa bungeni

MUUNGWANA BLOG / 13 hours ago



Naibu Spika Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa Kibamba Mhe. John Mnyika na Ester Bulaya kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge kwa kile alichodai kutoheshimu kiti cha Spika.

Naibu Spika ametoa maamuzi hayo jioni ya leo Mei 9, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19 ambapo Mbunge John Mnyika alisimama akitumia kanuni ya 69(1), kutaka kuahirishwa kuhitimishwa kwa hoja ya wizara ya Maji na Umwagiliaji ili apewe nafasi ya kutoa hoja yake ya kwanini bajeti ya wizara hiyo isipitishwe na Bunge.

Mara baada ya kauli hiyo, Dk Tulia alisimama akitumia kanuni ya 69(2), kusema kama Spika atakuwa na maoni kwamba kuwasilishwa kwa hoja hiyo ni kinyume cha uendeshaji bora wa shughuli za Bunge, atakataa kuitoa ili ijadiliwe.

Mbali na Mnyika Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amemtoa pia ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kwa kutoheshimu kiti cha Spika.
 
Yanga yakiri kupitia kipindi kigumu

MUUNGWANA BLOG / 13 hours ago



Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imefunguka na kukiri kuwa inapitia katika changamoto kubwa kutokana na baadhi ya wachezaji mpaka kuwa majeruhi hali ambayo inawasababisha kukosa kushiriki katika michezo mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten leo Mei 09, 2018 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matayarisho yao kuelekea mtanange wao dhidi ya Tanzania Prisons mchezo utakaochezwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

"Zipo changamoto kadhaa tunazozipitia kama timu kwa maana ya kwamba tumekuwa na wachezaji wengi majeruhi kwa muda mrefu na mpaka sasa tunaelekea ukingoni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara wapo ambao wamesharejea katika kikosi na wengine wakiwa bado hali zao hazijaimarika sana kwa maana kwamba bado hawajawa tayari kwenye kupambana", amesema Dismas.

Yanga imekwenda Mbeya ikiwa kwenye mtego wa kutoa ubingwa kwa Simba endapo itatoa sare au kufungwa kwenye mchezo huo itakuwa imevua rasmi taji la ligi kuu baada ya kudumu nalo kwa misimu mitatu mfululizo.
 
Kanuni 4 Za kujenga Mahusiano bora ya kimapenzi

MUUNGWANA BLOG / 12 hours ago




Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in . Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na mtakapoishi.

1. Kuwa na muonekano chanya kwa mpenzi wako.
Ukiwa ni mtu wa kuangalia mabaya/kasoro sana kwa mpenzi wako kuliko mazuri yake hautakuja kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu hata siku moja, utaendelea kubadilisha Wmwanaume / Wanawake kila siku na mwisho wa siku utajiona huna bahati kwenye mapenzi na wakati Unayeyaharibu mapenzi yako ni wewe Mwenyewe.. kakuna asiye na kasoro (Ukiwemo Wewe Mwenyewe).

Kwa hiyo muonyeshe mpenzi wako mapenzi bora na umrekebishe pale anapokosea Bila Kuwa Na Lawama Mara Kwa Mara, Kuna Makosa Mengine Ni Hakuna binadamu asiyefahamu nini maana ya mapenzi na kama wapo basi ni wachache sana na wanaweza kuwa hawafahamu kwa maneno lakini kivitendo wanakuwa wanafahamu aidha kwa kuona, kusikia na hata kwa wao wenyewe kushiriki kwenye mapenzi hayo.

Na hakuna binadamu yeyote asiyependa kupenda au kupendwa, wote tunapenda kupenda na pia tunapenda kupendwa in return. Na siku zote ukipenda na usipopendwa pale unapopenda huwa inakuwa ni huzuni sana na wengine hufikia hatua mbaya sana za kufikiria mengine mengi tu ya hatari pale mapenzi yanapokuwa machungu kwao.

Hii ndio sababu wengi wetu huwa tunakaa pale tunapoona kweli kuna mapenzi na si kukaa pale ambapo unaona unadanganywa au kuzungushwa kila siku. Lakini kuna wakati tunaweza kujikuta hata pale tunapopenda na kupendwa pia panaharibika baada ya muda na kunakuwa na ugomvi na kukosa maelewano baina yenu na wakati mwingine usifahamu kwa nini hamuelewani au ukaelewa lakini ukakosa njia za kutatua.

Zifuatazo ni baadhi tu ya njia mbalimbali za kufanya ukae na mpenzi wako kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mkafurahia mapenzi yenu popote pale mtakapokuwa na mtakapoishi.

1. Samehe na kusahau.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote alilokosa basi hakikisha umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione kuwa hakusamehewa.

2. Mpe nafasi na uhuru mpenzi wako.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na kimaisha.anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo yake. usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.

Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.

3. Mfanye mwenza wako ajivunie kuwa nawe kila wakati.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye. Wapo wengi sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua.Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.

4. Msadie kwa khali na mali kila inapowezekana.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na kushuka miongoni mwa wapenzi na hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika hali ambayo hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote hakikisha wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi.

Sio matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo chanya inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe.Kama unampenda usione tabu kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa hiyo jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na mpenzi wake.

Yapo mambo mengi sana ambayo kama mkiyafanya kwenye mapenzi basi uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha sana ingawa hapa nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia sana kwa wote walio kwenye mahusiano .

Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku moja, unapoona wapenzi wengi wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu wanavumiliana kwa mengi na kusameheana kwa mengi. Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya. Kanuni sita (6) za kudumu katika mahusiano ya kimapenzi
 
Chanzo cha Kipanda Uso na Tiba zake

MUUNGWANA BLOG / 12 hours ago



Kuumwa na kichwa kumegawanyika sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni ashirio la matatizo ya kiafya ambayo yame-advance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.

Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo:

Mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.

Baadhi ya neva za fahamu zilizoko usoni


Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazina mifumo ya fahamu ambayo inahisia.

Mambo haya 12 yanayo yanahusika sana.

1. Nervous tension headaches;
Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , ounguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2. Cluster headaches;
Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3. Hangover headaches;
Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4. Exertion headaches;
Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5. Caffein headaches;
Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6. Sinus headaches;
Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7. Bilious headaches;
Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8. Hunger headaches;
Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9. Eyes ram headaches
Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10. Menstrual headaches;
Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11. Arthritis headaches;
Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12. Hypertension headaches;
Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

Kabla ya kukupa dawa na ushauri wangu nina maswali nikuulize unijibu.
Je unapata Usingizi wa kutosha? Unalala usiku masaa mangapi? Je, unakunywa maji ya kutosha? Una miaka mingapi? Unapata haja kubwa ya kutosha? Nenda pia kapime macho yako na ukapime tena kwenye mishipa yako ya fahamu huenda una matatizo. Na kitu kingine unakuwa upo juani uwe unavaa kichwani kofia.
 
Malaysia yapata kiongozi mkongwe zaidi duniani aliyechaguliwa

MUUNGWANA BLOG / 2 hours ago



Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia Dr.Mahathir Mohamad amepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi mkuu uliofanyika katika hilo. Kiongozi huyo ameweza kukiangusha chama ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1957 ambacho kimekuwa kikidaiwa kujihusisha na nasuala ya rushwa na ufisadi.

Dr.Mahathir ameshinda kwa idadi ya uwingi kura,na kukibwaga chama cha Barisan Nasional kilichotawala kwa zaidi ya miaka 60.

Akiwa na umri wa miaka 92 Mhathir ameachana na kuitwa mstaafu na amerejea tena kuchukua nafasi ya mfuasi wake huyo wa zamani yaani Najib Razak ambaye utawala wake umekuwa na shutma kadhaa za rushwa.

Ibrahim Suffian, ni mtafiti wa masuala ya uchaguzi wa kujitegemea wa mjini Kuala Lumpur,anasema matokea haya yameleta mmshituko mkubwa.

"Tupo hapa tumekumbwa na mshangao kutokana na matokeo haya,ni jamba ambalo halikutarajiwa na ilikuwa vigumu sana kuweza kujua nani atabiri nani mshindi kwa kadri kura zilivyokuwa zikiendelea kuhesabiwa."Ibrahim

Malaysia katika utawala uliopita imeshuhudia kupanda kwa gharama za maisha na ongezeko la visa vya utengano wa kikabila,jambo ambalo Ibrahim Suffian anasema Dr Mahatir aliweza kuleta ushawishi mkubwa kwamaba anaweza kuleta mageuzi.

"Nafikiri jambo hili,na kufanikiwa kutekeleza mambo kadhaa yanayoonekana kuwa kikwazo.Jambo la kwanza ataunda muungano unaoshirikisha vyama vingine vya upinzani,na mbili nafikiri amewezakuwa na ushiwishi mkubwa kubainisha matatizo ya kisiasa ambayo yamekuwa yakiikabili Malaysia kwa takribani miaka 60 iliyopita,kama masuala ya kodi na mikasa ya rushwa ambayo ilimhusisha hata waziri mkuu pia."

Najib Razak kashindwa na mengi kwani pia anahusishwa na kashfa ya kudaiwa kujipatia kiasi cha dola 700 kutoka taasisi moja ya maendelea ya Malaysia na mamlaka zinaendelea kuchunguza kashfa hiyo.

Kufuatia ushindi wa Dr Mahathir, serikali imetangaza mapumnziko ya siku mbili ya kitaifa kwa siku ya Alhamis na Ijumaa.
 
Yanga yashuka dimbani kuivaa Prisons Leo ikiwa na wachezaji pungufu

MUUNGWANA BLOG / 23 minutes ago




Kikosi cha Yanga kinateremka dimbani Sokoine jioni ya leo kuvaana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Uongozi wa Yanga umesema unataka kutengeneza heshima hata kama wataukosa ubingwa wa ligi kwa kushinda mechi zote zilizosalia.

Yanga inashuka dimbani ikiwa pungufu kufuatia nyota wake kadhaa kusalia jijini Dar es Salaam ikilelezwa kuwa ni madai ya mshahara.

Msafara wa Yanga haujaweka wazi orodha ya kikosi kilichosafiri kwa ajili ya mchezo dhidi yao na Prisons utakaoanza saa 10 leo.

Timu zote mbili zimejivuna kupigania alama tatu kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka jijini Mbeya.
 
Sugu afunguka kuwasha moto Mbeya

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago




Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu'' amefunguka na kusema kuwa atawasha moto katika jiji la Mbeya Mjini pindi atakapotoka kutumikia kifungo chake cha miezi mitano jela ambapo sasa kinakwenda ukingoni.

Sugu amesema hayo kupitia kwa Mwenyekiti wa baraza la vijana la Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (BAVICHA) Taifa Patrick Ole Sosopi ambaye mwisho wa wiki iliyopita alipata fursa ya kumtembelea katika gereza la Rwanda.

"Siyo siri ni kwamba tunaamini mwezi huu watatoka wote ila Sugu anasema atawasha moto Mbeya, na kuwatumikia wananchi na kukutumikia chama mahali popote ambako chama kitamfanya aweze kwenda kwa kuwa yeye ni mjumbe wa kamati kuu, hivyo yapo mambo mengi naamini akitoka atayaeleza mwenyewe kwa undani zaidi, pia Masonga ameahidi akitoka atawaeleza wananchi ni jinsi ambavyo tunapaswa kupigania haki zetu na kuwa hatupaswi kuwa waoga nali tunapaswa kufanya harakati kwa njia nzuri na salama na kugusa maisha ya watanzania ambao tunawaongoza na kuwatetea" alisema Sosopi

Mbali na hilo Sosopi alieleza kuwa viongozi hao wametoa shukrani kubwa kwa watanzania pamoja na wanachama wa CHADEMA kwa jinsi ambavyo walikuwa wanakwenda kuwapa faraja kwa kuwaona magereza, hata hivyo Sosopi amedai kuwa viongozi hao mwezi huu wanaweza kutoka japo hajasema itakuwa lini na kusema kuwa watu wa magereza wao ndiyo wanajua siku gani na tarehe gani viongozi hao watatoka ndani ya mwezi huu.

"Tuwe na subira siyo kwamba ni siri lakini tuwe na subiri tunatambua kwamba viongozi wetu hawa wamebakisha muda mchache sana watatoka ni lini nafikiri hatupo tayari kueleza hilo kwani ni mapema zaidi ila tutawaeleza tu tutakapokuwa tunaona kuna sababu ya kuwaeleza ni lini watatoka lakni tunaamini ndani ya mwezi huu watatoka kwa sababu ni wakati muafaka, kama unavyojua sisi si wasemaji wa Magereza kwamba tunajua wanatoka lini, ila tunachojua watatoka ndani ya mwezi huu" alisisitiza Sosopi

Februari 26, 2018 Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi kwa jina maarufu Sugu na mwenzake Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walihukumiwa kwenda jela kwa miezi mitano kwa kosa la kumkashfu Rais John Pombe Magufuli.
 
Marekani yaomba Burundi ‘kuisamehe’ VOA

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago




Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Utangazaji wa Mashirika ya Serikali ya Marekani (BBG) ambayo inasimamia shirika la habari la Sauti ya Amerika (VOA), John Lansing amemuomba Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kutengua uamuzi wake wa kufungia matangazo ya VOA kurushwa nchini humo.

Wiki iliyopita Burundi ilifungia matangazo ya mashirika ya VOA na BBC kwa kipindi cha miezi sita kwa madai ya kukiuka maadili ya uandishi wa habari.

Lansing ameeleza kuwa bodi hiyo itaendelea kuwaunga mkono raia wa Burundi kwa kutoa matangazo ya kuaminika na yasiyopotosha.
 
Ryan Giggs amuombea Sir Alex Ferguson

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Meneja wa Wales Ryan Giggs anasema anatumai na anaomba meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson ataweza kupona uvujaji wa damu ubongoni.

Ferguson, mwenye umri wa miaka 76, bado yupo katika hali mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura siku ya Jumamosi.

Meneja huyo wa zamani alimruhusu Giggs wakati huo akiwana miaka 17 kucheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Manchester United mnamo 1991 na alikuwa katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za Ferguson na kushinda mataji ya Premier League.

"Sasa ni wakati wa kumuombea na kutamaini kuwa atapona kikamilifu," Giggs ameiambia BBC Wales.

"Amekuwa na ushawishi mkubwa katika kazi yangu ndani na hata nje ya uwanja.

"Najua upasuaji ulikuwana ufanisi - lakini yeye ni mpanaji na hilo ndilo linalonifanya nikafikiria kuwa ataweza kupona."

Meneja wa sasa wa Manchester United na mlinzi wa timu ya taifa ya England Phil Jones, pia ametuma ujumbe kama wa Giggs kwamba anamuombea Ferguson na amemtaja kama babake.

Jones alisajiliwa kutoka Blackburn na Ferguson akiwa na umri wa miaka 19 mnamo Juni 2011 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda cha mechi yake ya mwisho kabla astaafu mnamo Mei 2013 baada ya kushinda mataji 38 katika muda aliyohudumu wa miaka 28 katika klabu hiyo.

"Alinishukulia kama mtoto wake, na lilikuwa jambo la kushangaza," amesema Jones, mwenye umri wa miaka 26.

"Inahuzunisha lakini namjua, na atapambana vilivyo."

Michael Carrick, aliyecheza chini ya ukufunzi wa Ferguson kwa miaka 7 na anapokea ukufunzi wa wa klabu hiyo amesema amuhuzunishwa sana kusikia taarifa kuhusu Ferguson.

Mameneja katika ligi ya England akiwemo wa Arsenal, Arsene Wenger na wa Manchester City's Pep Guardiola, wote walituma ujumbe na maombi mwishoni mwa juma kwa Ferguson, ambaye anasifika kuwa Meneja mwenye ufanisi mkubwa katika historia ya soka Uingereza.

Wenger, ambaye anaondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, amemtaja Ferguson kama 'mtu mwenye matumaini ' huku Guardiola akisema anamfikira sana mkewe Ferguson Cathy na familia yake nzima akiwemo mtoto wao Darren, ambaye kwa sasa anaisimamia timu ya Doncaster Rovers.
 
Beki wa Arsenal kuwa nje ya dimba miezi sita

MUUNGWANA BLOG / 2 days ago



Beki wa klabu ya Arsenal, Laurent Koscielny, atakosekana nje ya dimba kwa muda wa miezi 6 baada ya kuumia mguu.

Koscielny aliumia mguu wake katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali katika UEFA Europa League dhidi ya Atletico de Madrid uliopigwa nchini Spain Alhamis ya wiki iliyopita.

Bei huyo ameumia zikiwa zimesalia wiki kadhaa tu kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza huko Russia.

Kwa mujibu wa Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema kuwa mchezaji huyo atakosa rasmi michuano ya Kombe la Dunia inayotaraji kuanza mwezi ujao huko Russia.
 
Back
Top Bottom