Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Serikali yatangaza ajira zaidi ya elfu sita

MUUNGWANA BLOG / 13 hours ago



Serikali kupitia Ofisi ya Rais –TAMISEMI imetangaza nafasi za kazi 6,180 katika sekta ya Afya ikiwemo Madaktari, Wafamasia, Wauguzi, Tabibu, Wahudumu wa afya nk, lengo likiwa kuhakikisha kuwa upungufu wa Watumishi wa ya afya unatatuliwa.

Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo amekaa mbele ya wandishi wa habari na kuzitangaza fursa hizo na kusema wajitokeze watu walio na sifa za taaluma hizo za afya na kuomba nafasi hizo ili waweze kuajiriwa na kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha Waziri Jafo amezitaja sifa za waombaji wanazotakiwa kuwa nazo kuwa awe Raia wa Tanzania, aambatanishe nakala ya vivuli vya vyeti halisi vya kidato cha nne na cha sita, aambatanishe kivuli cha cheti cha taaluma anayoombea ajira kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) au chombo kinachotambulika na serikali kinachotoa usajili nk.
 
UNICEF: Bado idadi kubwa ya watoto hawajawahi kunyonya maziwa ya mama

MUUNGWANA BLOG / 13 hours ago



Idadi ya watoto wanaokosa kunyonya maziwa ya mama bado ni kubwa hususan miongoni mwa nchi tajiri duniani umesema uchambuzi mpya uliotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Uchambuzi huo unasema takribani watoto milioni 7.6 kote duniani hawanyonyeshwi mazima ya mama kila mwaka. Maaike Arts ni mtaalamu wa masuala ya lishe wa UNICEF mjini New York amesema changamoto kubwa kwa wanawake ni msaada na será.

“Wanawake wanahitaji msaada ili kunyonyesha, ambao unajumuisha sera. Inamaanisha msaada kutoka kwa wahudumu wa afya, mila na desturi, jamii ambazo zinasaidia wanawake. Hivyo msaada huu hivi sasa haupatikani ipasavyo katika nchi za kipato cha juu ukilinganisha na zile nchi za kipato cha chini.”

Uchambuzi huo wa UNICEF unaonyesha kwamba ingawa unyonyeshaji wa maziwa ya mama unaokoa maisha, kulinda watoto na mama dhidi ya maradhi hatari na kuongeza ufahamu wa kiakili wa mtoto, inakadiriwa kwamba asilimia 21 ya watoto katika nchi tajiri hawajawahi kunyonyeshwa. Na katika nchi za kipato cha chini na wastani kiwango ni asilimia 4. Akisistiza umuhimu wa kunyonyesha Bi Arts amesema

“Tunachofahamu ni kwamba unyonyeshaji ni muhimu sana kwa watoto na kina mama pia. Kwa watoto unapunguza kiwango cha vifo vya mapema , unazuia idadi kubwa ya magonjwa kana kichomi na kuharisha, lakini pia fursa ya kuwa tipwatipwa. Na kwa kina mama tunaona kwamba unapunguza nafasi ya kupata saratani ya matiti, pia unalinda dhidi ya saratani ya mirija ya uzazi na kisukari.”

Ameongeza kuwa ili kuchagiza kina mama kunyonyesha hasa katika nchi tajiri, ni kuongeza ufadhili , sera za likizo ya uzazi, kuruhusu unyonyeshaji katika maeneo ya kazi, sera za kupunguza biashara ya maziwa mbadala, chupa na pia msaada unaohitajika pindi mama anapojifungua.

Baadhi ya nchi zilizo na kiwango cha juu cha unyonyeshaji watoto ni Bhutan,Madagascar na Peru zote zikiwa na asilimia 99, wakati nchi tajiri kama Irelani ni asilimi 55, na Marekani asilimia 74 , Marekani pia inashikilia theluthi moja kati ya watoto milioni 2.6 ambao hawajawahi kunyonyeshwa duniani.
 
Rais Trump atangaza kujitoa katika mkataba wa nyuklia

MUUNGWANA BLOG / 13 hours ago



Hatimaye Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuitoa nchi yake katika mkataba wa kimataifa wa mpango wa Nyuklia wa Iran.

Rais Trump ameutaja mpango huo kuwa si salama kwa Marekani na raia wake, huku akisema kuwa mpango huo ni kero kwa taifa la Marekani.

Licha ya wito kutoka jumuiya ya kimataifa, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, Donald Trump ametangaza kujitoa kwenye mkataba wa Vienna, uliyosainiwa mwaka 2015

Donald Trump amesema mpango huo hauwezi kuleta amani na usalama hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015 chini ya utawala wa aliyekuwa rais taifa hilo Barack Obama.

Nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Israel na Saudi Arabia wamepongeza hatu hiyo ya rais wa Marekani.

Makubaliano hayo yanaondoa vikwazo dhidi ya Iran kwa kubadilishana na ahadi kuhusu mpango wake wa nyuklia.
 
Simba Mabingwa wapya wa ligi kuu Bara

MUUNGWANA BLOG / 15 hours ago



Simba wanakabidhiwa ubingwa wakiwa mjini Singida hata kabla ya kuivaa Singida katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, keshokutwa Jumamosi.

Hii inatokana na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga kufungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Kufungwa kwa Yanga kuinaifanya ibaki na pointi 48 katika nafasi ya tatu, Azam FC katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 na Simba sasa wanachukua ubingwa wakiwa na pointi 65.

Simba wanachukua ubingwa wakiwa na pointi tatu mkononi.
 
Simba Mabingwa wapya wa ligi kuu Bara

MUUNGWANA BLOG / 15 hours ago



Simba wanakabidhiwa ubingwa wakiwa mjini Singida hata kabla ya kuivaa Singida katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara, keshokutwa Jumamosi.

Hii inatokana na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga kufungwa kwa mabao 2-0 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Kufungwa kwa Yanga kuinaifanya ibaki na pointi 48 katika nafasi ya tatu, Azam FC katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 na Simba sasa wanachukua ubingwa wakiwa na pointi 65.

Simba wanachukua ubingwa wakiwa na pointi tatu mkononi.
Imaonekana unapenda kutumia / kumiliki blogu ukihitaji nitafute pm tuongee. [emoji4] [emoji123]
 
Yanga hoi kwa Tanzania Prisons

MUUNGWANA BLOG / 15 hours ago



Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imekabidhi rasmi ubingwa kwa watani wao wa Jadi, Simba SC baada ya kuchapwa bao 2-0 na wenyeji wao Tanzania Prisons 'wajela jela' mchezo ulichezwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya jioni ya leo Mei 10, 2018.

Bao la kwanza la wajela jela limepatikana mnamo mwa dakika 58 katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Eliuter Mpepo baada ya mchezaji wa Yanga Thaban Kamusoko kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Kama hiyo haitoshi ilipofikia dakika 83 za mchezo huo Tanzania Prisons walipata bao la pili kupitia Juma Abdul krosi iliyotengenezwa na Mohamed Rashis baada ya vuta ni kuvute na walinzi wa lango la Yanga.

Kutokana na ushindi huo wa Tanzania Prisons wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga yanaipa rasmi Simba SC ubingwa wa moja kwa moja wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/ 2018 na kuifanya timu hiyo kunyakua kikombe hicho mara ya 19 na mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni mwaka 2012.
 
Back
Top Bottom