Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Simba SC yaelekea Mkoani Singida Leo

MUUNGWANA BLOG / 21 hours ago




Kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kimeondoka jijini Dar es Salaam asubuhi hii na kuelekea mkoani Singida, tayari kwa mchezo wa Ligi kuu Mei 13, 2018 dhidi ya Singida United.

Hayo yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na Meneja wa wekundu wa Msimbazi Simba leo Mei 10, 2018, Richard Robert na kusema kikosi chake kimeanza safari ya kuelekea mkoani Singida kwa kupitia Dodoma.

"Tumeanza safari yetu kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Singida United, safari yetu tutapitia mkoani Dodoma na kuweka kambi ya muda kabla ya kwenda Singida", amesema Richard.

Simba yenye alama 65 inahitaji alama moja tu ili kuweza kuwa bingwa wa VPL msimu huu wa mwaka 2017/18 kwani itafikisha alama 66 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga wala Azam FC ambao ndio wapo nyuma ya Simba kwa mujibu wa msimamo wa ligi. Sare yoyote kwenye mchezo na Singida itaipa Simba ubingwa.
 
IMG-20180103-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom