Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Gor Mahia kucheza dhidi ya Hull City

MUUNGWANA BLOG / 15 hours ago



Mabingwa wa ligi ya kandanda nchini Kenya Gor Mahia watakabiliana na klabu ya Uingereza Hull City jijini Nairobi.

Hull City, ambayo hushiriki katika ligi ya daraja la pili EFL nchini Uingereza wanatarajiwa kuwasili siku ya Ijumaa kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumapili katika uwanja wa Kasarani..

Ziara ya klabu hiyo barani Afrika inafadhiliwa na kampuni ya Kamare ya Sportpesa kutoka kenya ambayo ni mfadhili wa timu tatu.

Tayari Hull City imetuma ujumbe unaoongozwa na mchezaji wa zamani Dean Windass.

''Ijapokuwa baadhi ya wachezaji huenda wamechoa kutokana na msimu huu nina hakika kwamba wataonyesha mchezo mzuri'', alisema Windas alipopwasili Kenya.

Ziara hiyo ya Hull City inajiri mwaka mmoja baada ya Gor Mahia kucheza na kupoteza 2-1 dhidi ya timu ya ligi ya Premier nchini Uingereza Everton katika mechi nyengine ya kirafiki iliochezwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam.

Mwaka uliopita Hull City iliochezesha vijana wadogo iliishinda timu Kenya All Star 2-1 nchini Uingereza.

Hull City ilishushwa daraja kutoka katika ligi ya UIngereza mwisho wa msimu 2016/2017na sasa wako katika nafasi ya 18 katika orodha ya timu 24 za daraja la pili huku ikiwa imesalia mechi mbili pekee msimu kukamilika.

Gor Mahia ilijikatia tiketi ya kucheza dhidi ya klabu ya pili ya Uingereza chini ya mwaka mmoja baada ya kuishinda klabu ya AFC Leopard 5-4 kwa njia ya penalti katika uwanja wa Afraha.


 
VIDEO: " Hata kwa Nyerere Hakuna Maji, Bora Wakoloni Kuliko CCM"

MUUNGWANA BLOG / 22 hours ago




Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche amesema mipango mingi ya Serikali inafeli kutokana na kuwa na mipango ya muda mfupi, Heche amesema Serikali ya CCM imeshindwa kuendeleza hata mabomba yaliyoachwa na wakoloni.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KUSUBSCRIBE



 
VIDEO: UFISADI! Nkamia Aibua Wizi Mwingine Bungeni

MUUNGWANA BLOG / 22 hours ago




Mbunge wa jimbo la Chemba, Juma Nkamia (CCM), ametaja ufisadi na wizi uliopo kwenye miradi huku akitaka kuundwa kwa tume huru ya bunge kuchunguza miradi hiyo. Nkamia amesema hayo wakati akichangia mjadala wa wizara ya maji kwenye bunge la bajeti linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KUSUBSCRIBE



 
Bunge lataka tende zifutiwe kodi mfungo wa Ramadhani

MUUNGWANA BLOG / 24 hours ago




BUNGE limeendelea kuibana serikali itekeleze agizo la kuondoa kodi kwenye tende, ili kuwawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kupata bidhaa hiyo kwa urahisi katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, aliigiza serikali kufanyia kazi agizo hilo alipotolea ufafanuzi mwongozo ulioombwa kwake Hamidu Bobali bungeni jijini hapa jana asubuhi.

Mbunge huyo wa Mchinga (CUF), alisimama na kuomba Bunge liahirishe shughuli zake za jana na kujadili hoja hiyo kwa muda wa dakika 30 kwa kuwa licha ya wabunge kadhaa akiwamo Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea na Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe kuiomba serikali iondoe kodi kwenye tende katika vikao vilivyopita, bado haijatekeleza.

Alisema tende katika nchi za Kenya, Zanzibar na Msumbiji zimefutiwa kodi katika kipindi cha kuelekea mfungo huo, lakini Tanzania bado haijachukua uamuzi huo.

“Sasa, Mwezi wa Ramadhani unaanza wiki ijayo na makontena yapo kwenye meli bandarini ambayo yametolewa kwa msaada wa mali za wakfu, watu wanajichangisha mali za wakfu zinaletwa na wao wanatafuta swawabu. Sasa naliomba Bunge walau nusu saa, kwa sababu jambo hili linaiaibisha Tanzania,” alisema.

Akimjibu mbunge huyo, Dk. Tulia alisema kuwa jambo hilo limeshazungumzwa na utaratibu wake upo kisheria, hivyo serikali ina wajibu wa kuliangalia.

“Nadhani serikali ifanyie kazi jambo hili ione namna bora ya kushughulikia, kama ambavyo Bobali ametaja mifano ya huko kwingine sijasoma sheria zao, lakini sheria tunatunga wabunge, ila watekelezaji serikali, upande wa watekelezaji mwangalie namna ya kushughulikia jambo hili ili Mwezi wa Ramadhani unapokuja, wenzetu wenye imani ya Kiislamu waweze kupata hizo huduma ambazo zipo kiutaratibu," alisema.
 
Naibu Spika aagiza wateja wa benki iliyofungwa walipwe

MUUNGWANA BLOG / 24 hours ago




NAIBU Spika, Dk. Tulia Ackson, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutatua changamoto ya kutolipwa kwa wateja wa benki ya FBME ambayo imefungwa na Benki Kuu (BoT).

Kiongozi huyo alitoa agizo hilo bungeni jijjini Dodoma jana alipokuwa anajibu mwongozo ulioombwa kwake na Mbunge wa Muyuni, Jaku Hashim Ayoub (CCM).

Mbunge huyo alitaka mwongozo wa Kiti cha Spika, ili serikali ieleze ni lini hasa wateja wa benki hiyo kwa upande wa Zanzibar watalipwa fedha zao.

“Kwa sababu amelizungumza hapa na ni wananchi wanaopata tabu, Wizara ya Fedha imesikia, impatie Mheshimiwa Jaku ufafanuzi kuhusu jambo hili ili na yeye aweze kuwafafanua wapigakura wake," alisema.

Kabla ya kuombwa mwongozo wa Kiti cha Spika kuhusu jambo hilo, Jaku kuwa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, wateja wa benki hiyo kwa upande wa Zanzibar hawajalipwa chochote, “Nataka kujua wateja hawa watalipwa lini na je, fedha zao ziko salama kweli?" Jaku alihoji.

Novemba mwaka jana, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, alisema serikali imetenga Sh. bilioni 728 kwa ajili ya kuwafidia wateja 695 wa benki hiyo.

Akizungumza bungeni kipindi hicho, Dk. Kijaji alisema malipo kwa wateja hao yanafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 39 cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

“Serikali haina mpango wa kumwonea mteja yeyote. Madeni yote yatakusanywa na fedha italipwa kwa wateja kulingana na kiwango walichoweka na kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Serikali inalifanyia kazi suala hili kwa uangalifu mkubwa," alisema.

Dk. Kijaji alitoa maelezo hayo bungeni alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahmed (CUF), ambaye alitaka kujua malipo kwa wateja wa benki hiyo yatafanyika lini baada ya leseni yake kufutwa na serikali mwaka jana.

Mei 8, mwaka jana, Benki Kuu (BoT) ilitangaza kuzuia shughuli za FBME na kuiweka chini ya uangalizi maalum baada ya serikali ya Marekani kuituhumu benki hiyo kujihusisha na utakatishaji mkubwa wa fedha.

BoT iliingilia utendaji wa benki hiyo Julai 2014 kufuatia ripoti ya Mtandao wa Udhibiti wa Fedha Haramu wa Marekani (U.S. Treasury’s Financial Crimes Enforcement Network -FinCEN) kuitaja benki hiyo kuwa sehemu ya taasisi kubwa za utakatishaji fedha.

Benki hiyo ilifungua mashtaka kupinga tuhuma hizo, lakini mahakama ya Marekani ilitoa uamuzi uliokuwa upande wa FinCEN Aprili, ikiruhusu kufungwa kwa mfumo wa benki hiyo Marekani.
 
Pluijm afunguka kulipa kisasi kwa Simba

MUUNGWANA BLOG / 24 hours ago




KOCHA wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuelekea kwenye mechi yao dhidi ya Simba itakayopigwa kwenye Uwanja wa Namfua, amesema kuwa lazima walipe kisasi kwa wapinzani wao hao.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Singida United ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwao kulipa kisasi kwa wapinzani wao hao waliowafunga mabao 4-0.

“Hii ni nafasi nzuri kwetu kulipa kisasi cha 4-0 tulipokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani hivyo na sisi tumejiandaa kulipa katika uwanja wetu wa nyumbani, kwa sasa sisi hatufikiri mechi yetu ya fainali na Mtibwa kwani ipo mbali, hivyo tunaangalia hii ya Simba,” alisema Pluijm.
 
Chanjo ya Ukimwi yagawiwa bure

MUUNGWANA BLOG / 24 hours ago




JITIHADA za serikali katika kupunguza makali ama kutokomeza kabisa ugonjwa wa Ukimwi zimezidi kuleta matumaini, baada ya kutambulisha chanjo ya bure ya dawa ya kukinga mtu asipate maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Dawa hiyo iitwayo ‘dawa kinga’ ilitambulishwa jana, itaanza kusambazwa katika mikoa ya Mbeya na Songwe.

Utambulisho wa dawa hiyo ulifanyika jijini Mbeya kwa viongozi mbalimbali wakiwamo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na masuala ya Ukimwi katika mikoa hiyo miwili.

Akizungumza kuhusu dawa hiyo, mkurugenzi wa asasi iitwayo HJFMRI ambayo ndiyo iliyopewa kazi ya kusambaza dawa hizo kwa niaba ya serikali, Joseph Chintowa, alisema dawa hiyo ina uwezo wa kumkinga mtu asipate maambukizi ya VVU kwa zaidi ya asilimia 90, ikiwa itatumika kwa ufasaha.

Alisema mtu ambaye anastahili kutumia dawa hiyo ni yule aliyepima na kuonekana hajapata maambukizi ya VVU, lakini yuko kwenye hatari ya kupata maambukizi.

“Kabla ya kutumia dawa hizi unatakiwa kupimwa na ikionekana hujaambukizwa, unakuwa na sifa ya kutumia dawa kinga, na wale ambao watabainika kuwa tayari wana maambukizi, hawastahili kutumia dawa hizi,” alisema Chintowa na kuongeza:

“Badala yake watapewa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) kwa ajili ya kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi.”

Kwa mujibu wa Chintowa, kwa kuanzia, dawa kinga itaanza kutolewa kwa watu walio kwenye makundi hatarishi ya kupata maambukizi mapya kama vile watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, mabinti wanaofanya biashara ya ngono na watu wanafanya mapenzi ya jinsia moja.

Chintowa alisema hadi sasa wataalamu wa afya wapatao 42 na asasi 118 zisizo za kiserikali kutoka mikoa ya Mbeya na Songwe wameshapewa mafunzo maalum kwa ajili ya usambazaji wa dawa kinga kwa watu walio kwenye makundi hatarishi kuambukizwa VVU.

Alisema zoezi la utoaji wa dawa kinga linakwenda sambamba na uhamasishaji watu kujipima wenyewe VVU, ambapo vipimo kwa ajili hiyo vitatolewa kwa yeyote anayetaka kujipima afya mwenyewe.

MWAKILISHI WA WIZARA
Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Aafke Kinemo, aliwataka viongozi kuhamasisha jamii kwenye maeneo yao kutumia dawa hizo, ili dhamira ya kupunguza maambukizi mapya kwenye jamii iweze kufanikiwa.

Alisema wakuu wa wilaya, wanasiasa, viongozi wa dini na wa jadi wapo kwenye nafasi nzuri ya kuhamasisha wananchi kutumia dawa hizo na hatimaye kujikinga wenyewe na maambukizi ya VVU.

MWAKILISHI WA UN
Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Kinga na Tabia, Dk. Eniko Akom, alikemea suala la imani potofu dhidi ya huduma hizo akisema katika baadhi ya nchi imekuwa ni kikwazo kwa watu kujitokeza kuzitumia.

“Naomba niseme jambo, katika nchi nyingi watu wana imani potofu, baadhi yao wanakataa kutumia dawa hizi kwa kuhofia mimba na wengine wanadhani wakizitumia wanakuwa sawa na watu walioambukizwa Virusi vya Ukimwi, hizi ni imani potofu tuziache,” alisema Dk. Akom.

Badala yake alisema dawa hizo zikitumika kwa usahihi, zinao uwezo wa kumkinga mtu asipate maambukizi ya VVU na pia zitamkinga hata mtoto aliye tumboni asiambukizwe, hivyo ni dawa ambayo jamii ikiipokea vizuri inaweza kutokomeza kabisa Ukimwi.

KAULI YA RC MBEYA
Mgeni rasmi kwenye utambulisho wa dawa kinga, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, aliwasisitiza wataalamu wa afya na viongozi kwa ujumla kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwenye jamii dhidi ya huduma hizo, ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya dawa kinga pamoja na watu kujipima VVU wenyewe.

Alisema kama watu hawatakuwa na elimu ya kutosha, wanaweza kujikuta wanatumbukia kwenye matatizo makubwa, hivyo ni muhimu kabla ya kuruhusiwa kutumia dawa kinga au mtu kujipima mwenyewe kama ana maambukizi ya VVU akapewa elimu ya kutosha.

“Sio kila mtu anatakiwa kutumia dawa kinga, pia ni hatari mtu kwa mara ya kwanza akajipima mwenyewe kama ana maambukizi kwani endapo akakuta ameathirika anaweza kijidhuru mwenyewe, hivyo nadhani mnapaswa kwanza kutoa elimu ya kutosha kabla watu hawajaanza kutekeleza afua hizi,” alisema Makalla.

Mkoa wa Mbeya ni watatu kwa kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU nchini kwa kuwa na asilimia 9.7 ya maambukizi, ukitangulia Mkoa wa Njombe wenye asilimia 14 na Iringa wenye asilimia 11, Wastani wa kitaifa wa kiwango cha maambukizi ya VVU kwa sasa ni asilimia 4.5.

Hii ni mara ya pili kuzinduliwa chanzo ya Ukimwi. Miaka nane iliyopita chanjo nyingine ilizinduliwa na walioanza kufanyiwa majaribio ni askari.
 
Sugu afunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela

MUUNGWANA BLOG / 21 hours ago




Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ambaye ameachiwa huru leo kutoka gerezani alikofungwa akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutoka jela.

Akizungumza na East Africa Radio, Sugu amesema hakuwa anajua kama anaachiwa mpaka pale alipofuatwa na polisi kuambiwa ajiandae, na hajui imekuwaje mpaka akaachiwa sasa kwani ilijulikana ataachiwa huru mwezi wa 6.

“Watu wote walikuwa wanatarajia nitoke mwezi wa 6, lakini ghafla hapo jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi natakiwa niachiwe, kutoka nje nikakuta askari wengi na nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimin a mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maafisa magereza watano wakatupeleka mpaka nyumbani na kutukabidhi kwa familia”, amesema Sugu.

Sugu ameendelea kusema kwamba..."watu wanauliza imekuwaje lakini mimi nawaambia sijui kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi kama mimi ninachoamini sikutakiwa kuwa magereza in the first place, utumishi uko pale pale kwa level ile ile tulikuwa na exposure sasa hivi tumeongeza experience”.

Wawili hao wameachiwa huru leo kutoka gereza kuu la Ruanda mkoani Mbeya walikokuwa akitumikia kifungo chao cha miezi mitano, jambo ambalo limewashtua wengi kwani inaaminiwa muda wake ulikuwa bado haujaisha.
 
Aisee! Watumie tu.
 
Maneno ya Nape baada ya Sugu kuachiwa huru

MUUNGWANA BLOG / 21 hours ago




Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amekaribisha uraini Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gereza la Ruanda alipokuwa akitumikia kifungo chake .

Nape amesema kuwa anakumbuka Mbunge huyo ambaye pia ni msanii aliwahi kuimba juu yake wakat alipoanza siasa.

“Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter.

Sugu na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…