Miongoni mwa wanufaika wa miswada hiyo walikuwa ni kampuni ya saruji ya Dangote Liberia, TIDFORCE/LICEMCO, Nimba Rubber Incorporated (NRI), Menejimenti ya Usalama Barabarani Liberia na Marekebisho ya Makubaliano ya Firestone. Miswada hiyo na mingine iliwasilishwa na Ellen siku za mwisho.
Rais Weah amesema makubaliano hayo yalipitiwa upya na Kamati Maalumu ya Rais ya Marekebisho (SPRC) kufanya tathimini na kujihakikishia ikiwa yalikuwa yanaendana na taratibu na matakwa yaliyopo kwa Sheria za Liberia.
Hata hivyo alisema, matakwa ya kisheria katika makubaliano yaliyotajwa hayakuzingatiwa rejea ikiwa ni Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2010 ambayo amesema ilikiukwa.