Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Visheti vilain vitamu _MAHITAJI_ •Mayai 4 •Samli robo (250gm) •Unga wa ngano kilo moja •B.p kijiko kimoja tbs(usikujaze sana) •Maziwa kikombe kimoja •Arki •Sukar nusu iliyosagwa _MATAYARISHO_ Chukua bakuli weka samli, maziwa, na mayai saga. kisha weka unga kidogo kama nusu kikombe , saga hadi mchanganyiko wako uwe smoothy Kisha weka b.p, vanilla na chumvi kiduchu na sukar kiduchu kama utapenda, kisha weka unga wa ngano , kanda unga wako. Kata vishet vyako shape uipendayo Teleka karai jikoni kaanga vishet vyako kwa moto wa wastan usiwe mwingi sana na usiwe kidogo sana hadi viwive. Epua visheti vyako kisha weka katika sukar ya unga uliyoisaga (garagiza kama donut) Tayar kwa kuliwa,
 
*Bread pudding* Bread pudding : katakata vipande ndogondogo mkate aina yeyote kama scones vipande tano, au slice za mkate kama 12, tia kwenye mkebe ya kuokea tia zabibu kavu kiasi unapenda. Changanya vizuri. Weka kando. kwenye bakuli kubwa piga nusu lita ya maziwa, mayai 4 kubwa, 3/4 C sukari au unavyopenda, vanilla kijiko moja ya kula, vijiko tatu ya kula siagi iliyoyayushwa. Piga mpaka zichanganyike vizuri, mimina kwenye mkate, changanya pamoja vizuri, nyunyuzia sukari juu ukipenda. oka mpaka iive, dakika 35-40 moto ya kati. SAUCE YA CUSTARD: Changanya vikombe tatu ya maziwa pamoja na vijiko 2 1/2 ya kula ya custard poda, sukari unavyopenda, kijiko moja ya chai iliki. Koroga pamoja kwa moto ya kati, mpaka ianze kuwa nzito. Epua kisha serve na pudding ikiwa moto.
 
KASHATA ZA MAZIWA(FUDGE) Siagi 1/2 kikombe Sukari kikombe 1 Maziwa mazito (condensed milk) kikopo 1 Maziwa ya maji 1/2 kikombe Vanilla kijiko 1 JINSI YA KUPIKA 1.Weka sufuria jikoni ikipata moto weka siagi kisha tia sukari koroga tia vanilla ,maziwa ya maji na maziwa mazito kisha koroga kwa dakika 10 usiachie mpaka siagi iyeyuke vizuri kisha epua 2.Paka tray au sinia mafuta kisha mimina mchanganyiko wako,uache kwa dakika 10 kisha weka katika fridge kwa masaa 6 itoe itakua tayari imeganda vizuri katakata vipande weka katika sahani tayari kwa kuliwa.Ni tamuuuu!!! ENJOY!!! NB: Waweza kuongeza chocolate ukipenda kwa kuikata vipande vipande na kutia katika mchanganyiko wako wakati ushaepua ili chocolate isiyeyuke.
 
SAMAKI WA KUPAKA. Samaki Uzuri akiwa mkubwa. nazi ya kibati 1 Somu tangawizi kitungu maki 1 pili X2 bogoa 1 pili X2 Ndimu 1 Chumvi Bizari nzima 1 Tungule 2 Bizari ya manjano. Vegetable mix powder (optional) METHOD Msafishe Samaki Uzuri mtie misingi (alama) mtie thomu tangawizi kipande chumvi . Bizari nzima na pilix2. mfunike wacha akole. Kwenye blande saga kitungu maji ,Tungule pilix2 boga, pilix2 kidogo,kotmiri ukipenda na kibati 1 cha nazi saga Uzuri iwe nzito. Mimina Kwenye sufuria tia ndimu na chumvi bizari ya maanjano pika moto mdogo mdogo hadi iwe nzito. mtie Samaki Kwenye grill au Kwenye mbano ukiwa unatumia makaa ndo anazidi kuwa mzuri. mchome hadi awive Uzuri ukiwa unamnyunyizia maji ya ndimu kila bada muda hadi awive na kukauka. akishawiva nakukauka chukuwa lile rojo la nazi kidogo mwagie kwa juu ikisha mrejeshe Kwenye grill akauke ikisha mgeuze upande wa pili mtie tena kidogo mwache akauke na ile nazi ingie ndani ya Samaki anakuwa anazidi kukolea. akishakauka. Mtowe mwagie lile rojo lilobakia lakin hakikisha lile rojo liko zito kama uji sio jepesi. likiwa jepesi itakuwa Samaki wa nazi tu sio wakupaka ule utamu utapungua. ejoy.
 
CAKE YA LOZZI kikombe 1 unga. kikombe 1 sukari kikombe fresh cream vijiko vidogo baking powder mayai 2 nusu kijiko vanilla FOR TOPPING vijiko vikubwa 2 fresh cream 50gm siagi 1\4 sukari Changaya vote kwenye sufuria wacha vichemke ikianza kuwa nzito zima jiko. METHOD Changanya vitu vote pamoja kwa blender au mchapo. mimina kwa tray choma kwa moto was 180° muda wa 30minutes au hadi iwive. ukishaitowa pale pale imoto tupia almond na mwagia cream. wachaipoowe kula.
 

Lower left - The "Turn and Bank Indicator" is a dual instrument which tells how fast you are changing the compass heading (rate of turn) and also whether you are in co-ordinated flight, This is also called the "Turn and Slip Indicator" or "Needle Bal
 
TAMBI NA NYAMA YA KUSAGA Mahitaji Tambi 1/2 pt Nyama ya kusaga 1/2 kilo Kitunguu maji 1 Kitunguu saumuu na tangawizi 1tsp Nyanya 3 Nyanya ya kopo vijiko 4 Royco 1tsp Beef masala 1tsp Curry powder 1tsp Chumvi Mafuta Karoti nusu Pilipili hoho nusu Limao NJIA Kangaa kitunguu maji kisha weke tangawizi na kitunguu saumu kaanga kidogo kisha weka karoti, pilipili hoho na nyanya ya kopo. Kisha weka viungo wako royco,curry powder,beef masala na nyama yako ya kusaga. Kisha weka tambi na changanya na mchanganyiko na uweke maji kufunika tambi weka chumvi na limao na kisha funika acha hadi maji yakauke na tambi ziiive. Epua na andaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…