Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kuku mzima (makange style) Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu nusu kijiko Tangawizi nusu kijiko Curry powder nusu kijiko Masala nusu kijiko Limao Nyanya 3 Karoti 1 Kitunguu maji 1 Pilipili hoho nusu Chumvi Mafuta Njia Pasua kuku katikati kisha mpake limao na chumvi na kisha acha nusu saa na kisha mkaange kuku mzima kwy mafuta mpk aive awe rangi ya kahawia Kisha pembeni anza kwa kuweka mafuta kidogo kwy sufuria kisha weka kitunguu maji acha iwe na rangi ya kahawia kisha weka kitunguu saumu tangawizi curry powder na masala na kaanga kisha weka karoti pilipili hoho na endelea kukaanga kisha weka chumvi na ikisha ivaa mweke kuku wako kwy huu mchanganyiko aingii pande zote za kuku na kisha epua Kula na chochote ukipendacho ugali wali chips