Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mpaka dakika hii kocha huyo bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akiwa katika uangalizi maalumu wa kitabibu.

Habari zilizojiri majuzi zimeeleza kwa sasa Fergie ameweza kuzinduka na amepata fahamu kiasi cha kuweza kukaa na kuzungunza na kuwasiliana na ndugu na jamaa wa karibu.
 
Alipozinduka tu aliulizia familia yake kuhusu timu ya Doncaster Rovers kama imeshinda. Hii ni timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England kwa bahati mbaya siku ya Jumamosi ilichapwa 1-0 na Wigan.

Inaelezwa kuwa upasuaji huo wa kichwa ulifanyika kwa mafanikio makubwa lakini bado atahitaji muda mrefu ili kuweza kuwa mwenye afya njema.
 
Leo nitalieleza tatizo hili la kuvuja damu katika ubongo na tutaelewa ni kwanini lilihitaji upasuaji wa dharula.

Kinachotoea damu inapovuja katika ubongo?

Inapotokea damu imevuja na kutuama na kuganda katika ubongo husababisha athari hasi katika tishu za ubongo kwa kuzifanya zivimbe, hali hii hujukina kitabibu kama Brain Edema.
 
Back
Top Bottom