Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1526187365002.jpg
 
Zikiwa zimepita siku tatu tangu Serikali ilipowaagiza wafanyabiashara wa mafuta ya uto (kula) kuanza kuyaingiza sokoni, hali ya upatikanaji wake siyo nzuri kutokana na kuendelea kupanda bei jijini Dar es Salaam.

Leo ndiyo siku ya mwisho tangu Serikali ilipotoa amri hiyo na kuanzia kesho huenda msako katika bohari na maghala ya wafanyabiashara hao ukaanza.
 
Akizungumza bungeni juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa muda wa hadi leo kwa wamiliki hao kuingiza sokoni bidhaa hiyo na kuonya kuwa iwapo hilo halitafanyika Serikali itaanza msako huo.

Jana, Mwananchi lilipita katika maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara wa mafuta wa jumla na rejareja jijini Dar es Salaam ambapo wengine walisema wamelazimika kuacha kuyauza na wale wanaoendelea nayo wamekuwa wakiyauza kwa bei ya juu.
 
Wale wanaositisha uuzaji huo walisema wanafanya hivyo kutokana na hofu ya kukosa wateja kutokana na kuuziwa kwa bei ya juu na wauzaji wakubwa itakayowalazimu na wao kupandisha bei.
 
Wale wanaositisha uuzaji huo walisema wanafanya hivyo kutokana na hofu ya kukosa wateja kutokana na kuuziwa kwa bei ya juu na wauzaji wakubwa itakayowalazimu na wao kupandisha bei.
 
Sijaweka mafuta ya uto hapa kwangu hii ni wiki sasa, hapo awali nilikuwa ninanunua dumu la lita 20 Sh54,000 ghafla ikapanda hadi Sh56,000 nikaamua kuacha kwa sababu nawafahamu wateja wa mtaa huu nikipandisha bei hawatanunua,” alisema Joyce Pius, mmoja wa wafanyabiashara hao.
 
Joyce alisema kutokana na kutouza mafuta hayo dukani kwake anakosa wateja wa bidhaa nyingine kama vile unga wa sembe, ngano, mchele na sukari.

Mfanyabiashara wa duka la jumla katika eneo maarufu la Kinondoni TX, Ally Salim alisema wakati mafuta yanapanda alikuwa na akiba ya kutosha kwenye ghala lao.
 
Aliongeza kuwa kwa sasa wananunua lita 10 ya mafuta hayo kwa Sh38,000 na kulazimika kuuza kwa kati ya Sh40,000 hadi Sh42,000 kulingana na umbali wanakoyanunua.

Mfanyabiashara wa duka la rejareja katika Kata ya Mzimuni, Lucy Lazaro alisema, “Nimenunua leo dumu la lita 20 kwa Sh64,000 kutoka Sh54,000 niliyonunua mwishoni mwa wiki iliyopita.”
 
Back
Top Bottom