Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tunalazimika kuuza chupa ya lita moja kwa Sh3500 hadi Sh400 kutoka Sh3200 ya awali na bado inakata. Hili dumu la lita 20 lina chupa za lita moja 20 tu, ukijumlisha kumwagika na kuwaongeza kidogo wateja unajikuta unabaki na chupa 18 na nusu au 19, hivyo ni hasara tu.”

Katika eneo la Temeke, mafuta ya kula nusu chupa yaliyokuwa yakiuzwa Sh500 sasa yanauzwa Sh700.
 
1526187304991.jpg
 
Mchuuzi wa mafuta na bidhaa nyingine katika eneo la Tandika Azimio, Abdul Hafidh alisema anafanya biashara hiyo kwa mazoea. “Kupitia mafuta nitauza unga wa ngano na dengu, mchele na sukari kwa sababu wateja wangu ni wauzaji wa vitumbua na mama lishe, hivyo nisipokuwa na mafuta ya kula na walizoa kununua hapa nitawapoteza, ”alisema Hafidh.
 
Wasambazaji wakubwa

Gazeti hili jana lilifika katika ofisi za kampuni Murzah Oil Mills zilizopo eneo la Kipawa kutaka kujua kama agizo la Waziri Mkuu limeanza kutekelezwa, lakini lilipokewa na walinzi waliolekeza kuonana na ofisa mmoja aliyetoa maelezo kuwa si msemaji na kutaka atafutwe msemaji ambaye ilielezwa yupo katika ofisi nyingine zilipo eneo la Masaki.
 
Naomba chukua namba hii ya msaidizi wake (wa bosi) ili uzungumze naye,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka kujitambulisha.

Hata hivyo, alipopigiwa msaidizi huyo alipokea na kutaka apewe muda ili awasiliane na bosi wake na kuahidi kutoa majibu baadaye. Hata hivyo, alipotafutwa tena simu yake iliita bila majibu yoyote.

Juhudi za kuwapata wasambazaji wengine wakubwa wa mafuta hazikuzaa matunda.
 
Back
Top Bottom