Mchuuzi wa mafuta na bidhaa nyingine katika eneo la Tandika Azimio, Abdul Hafidh alisema anafanya biashara hiyo kwa mazoea. “Kupitia mafuta nitauza unga wa ngano na dengu, mchele na sukari kwa sababu wateja wangu ni wauzaji wa vitumbua na mama lishe, hivyo nisipokuwa na mafuta ya kula na walizoa kununua hapa nitawapoteza, ”alisema Hafidh.