Mmoja wa wazazi wa watoto wanaodaiwa kupigwa, Muniko Sibora kwamba alisema Mei 7 mwalimu huyo alimpiga mwanaye baada ya kuvaa yeboyebo kutokana na kuwa na kidonda mguuni.
Pia, alisema aliwapiga watoto wa Mwita Nyasongo na Ngocho Matiku kwa kuwa hawakwenda na majembe kupalilia mahindi yake.
“Huyu mwalimu anachofanya siyo sahihi, anatakiwa ahame vinginevyo mambo yatamharibikia,” alisema.