Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1526281882850.jpg
 
BREAKING NEWS: Tarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba kuna fununu kuwa Muigizaji maarufu nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ameachiwa huru na inaripotiwa tayari ametoka Gerezani. : Chanzo chetu cha habari hakijaeleza kama ametoka kwa msamaha wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli uliotoka tarehe 26 mwezi wa 4 au alikata rufaa na ameshinda au yupo nje kutumikia kifungo cha nje kwa Mujibu wa Sheria.
duh!!
 
Mcheza filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu amebadilishwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Akizungumza na MCL Digital Jumatatu Mei 14, 2018, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje
 
Back
Top Bottom