Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waziri Ummy atoa Ufafanuzi kuhusu Upimaji wa UKIMWI bar kwa bar

MUUNGWANA BLOG / 20 minutes ago




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema utaratibu wa upimaji wa kifua kikuu na UKIMWI bar kwa bar sio wa lazima, ila watatumia ushawishi kuhakikisha wananchi wanapima na kujua afya zao.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi (NACP).

”Tutatekeleza mpango wetu wa kupima TB na UKIMWI kwenye bar ila hautakuwa wa lazima, tutakachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma hiyo” amesema Ummy.

Aidha ameongezea kuwa Wizara ipo katika mkakati wa kubadilisha sera na sheria za UKIMWI na kuruhusu mtu aweze kujipima mwenyewe na kutoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kujipima wenyewe bila ridhaa ya wazazi.

Hatua hizo ni kufuatia serikali kutaka kubainisha na kuwatambua watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na TB kauli ambayo ilitolewa Aprili 23 mwaka huu na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.
 
Tanzania yatinga fainali Kombe la Dunia

MUUNGWANA BLOG / 21 minutes ago




Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia kwa watoto walio kwenye mazingira magumu, imetinga fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya wasichana ya England.

Tanzania imefanikiwa kutinga fainali hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wasichana wenzao wa England, kwenye mchezo wa nusu fainali uliomalizika asubuhi ya leo huko jijini Moscow Urusi.

Timu hiyo inayoundwa na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa Kituo cha TSC cha Jijini Mwanza, saa watacheza fainali dhidi ya wasichana wa Brazil ambao nao wamefuzu fainali hiyo.

Tanzania ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo mwaka 2014 nchini Brazil, timu ya wavulana walio kwenye mazingira magumu ilichukua ubingwa kwa kuifunga Burundi.

Katika hatua za makundi, Tanzania ilicheza na timu za Urusi, Kazakhstan na Marekani katika hatua ya robo fainali na kisha leo kuitoa England kwenye nusu fainali.
 
Ndugulile: Ni kweli lipo ongezeko la matukio ya ubakaji

MUUNGWANA BLOG / 22 minutes ago




Serikali imesema inakemea vitendo vya udhalilishaji na ubakaji wa aina yeyote ambao wanafanyiwa watoto na wanawake huku wakiwataka wahanga wa matukio hayo kutokaa kimya bali wakatoe taarifa kwenye vyombo dola ili sheria zipate kuchukuliwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Dkt. Faustine Ndugulile Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 28 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum, Mwantumu Haji ambaye alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kupambana na wanaume wanaowadhalilisha watoto.

"Ni kweli lipo ongezeko la matukio ya ubakaji na udhalilishaji wa wanawake na watoto. Serikali inaendelea kuhamasisha utekelezaji wa sheria ya kanuni za adhabu sura Na. 16 na sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 na kuhimiza wazazi walezi, jamii na wahanga wa vitendo vya ukatili kutokaa kimya pindi wanapoona mtoto au mwanamke anafanyiwa vitendo hivyo ili kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale wote wanaotenda vitendo hivyo", amesema Dkt. Faustine.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri Dkt. Faustine ameendelea kwa kusema "katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2017, Jeshi la Polisi limeripotiwa kuwapo na jumla ya matukio 41,416 ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake lakini kati ya hayo matukio 13,457 ni ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na serikali inaendelea kukemea udhalilishaji na ubakaji wa aina yoyote kwa wanawake na watoto".

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa wananchi wote nchini Tanzania amewataka kuacha tabia ya kumaliza mashauri ya kesi yaliyopo kwenye vyombo dola katika ngazi za kifamilia.
 
Mwafrika ateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago




Raia wa Senegal Makhtar Diop ameteuliwa kuwa makamu wa rais wa Benki ya Dunia (WB) atakayekuwa anasimamia miundombinu.

Diop alitangazwa kushika nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa taasisi hiyo muhimu duniani.

Taarifa iliyotolewa na benki hiyo inasema Diop anayaanza majukumu hayo mapya baada ya kuwa Makamu wa Rais anayesimamia Afrika katika miaka sita iliyopita akifanikisha kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya Dola 70 bilioni za Marekani.

Ndani ya miaka hiyo sita, Diop alisimamia miundombinu ya usafiri na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), nishati na madini, fedha na ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPP).

‘Katika majukumu yake mapya, Diop atasimamia ufadhili wa miundombinu ya fedha katika ufanikishaji wa maendeleo endelevu hivyo kupunguza tofauti iliyopo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Uteuzi wa Diop anayetajwa kuwa miongoni mwa Waafrika 100 wenye ushawishi zaidi duniani utaanza July 1.
 
CBA kuwasaidia Watanzania kumiliki Nyumba

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago




BENKI ya CBA Tanzania, imeelezea dhamira yake ya kuwasaidia Watanzania kumiliki nyumba kupitia mpango mpya utakaotoa mikopo nafuu kwa wenye kutaka kumiliki nyumba.

Akiongea wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kama sehemu ya kukutana na wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Gift Shoko, alisema mpango huo utawaleta pamoja wenye ardhi, wajenzi na mkopeshaji.

“Chini ya mpango huu mpya, tutafanya kazi pamoja na wenye ardhi na wajenzi ili kuendeleza ardhi ambayo haijaendelezwa kwa kujenga nyumba ambazo baada ya kwisha tutawapatia wateja wetu mikopo na kuzinunua,” alisema.

Shoko alisema, takwimu zinazotolewa na Serikali zinaonyesha kuwepo kwa mamia na maelfu ya Watanzania wenye uhitaji wa kumiliki nyumba kila mwaka lakini wengi wao wamekuwa wakishindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kushindwa kumudu gharama za kununua nyumba.

“Tunachokifanya sasa ni kutoa mikopo nafuu ambayo itawawezesha Watanzania wenye ndoto za kumiliki nyumba kuweza kufanya hivyo kwa urahisi. Lengo letu ni kuona tunawawezesha Watanzania wengi zaidi kumiliki nyumba zao,” alisema.

Shoko alisema nyumba ni moja kati ya mahitaji ya msingi ya binadamu na benki ya CBA inajisikia furaha kuwa benki ya kwanza kutoa mikopo ya muda mrefu ya nyumba inayofika hadi miaka 20 na kusisitiza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa mikopo mingi zaidi ya nyumba.

“Dhamira yetu kwenye kuchangia uchumi wa Tanzania inaonekana kwenye uwekezaji na upanuzi tunaofanya kwenye huduma zetu zikiwemo za kidijitali. Mwaka 2017, wanahisa wetu waliongeza shilingi 16.72bn/- kwenye mjati wa benki,” alisema.

Alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kuwekeza nchini, Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla kwa kuwa inalenga kuwa benki kubwa barani Afrika.

Chakula hicho cha jioni ni ratiba ya kawaida ya benki hiyo kukutana na wateja wake kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya namna ya kuboresha huduma pamoja na kupata mrejesho kutoka kwa wateja wake.
 
Bukunyika mkubwa wewe [emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_20180512_224021_807.jpg
 
At least 37 Palestinians have been killed and 1,300 wounded by Israeli troops in clashes on the Gaza border, Palestinian officials say.
The violence comes ahead of the opening of the US embassy in Jerusalem, which has infuriated Palestinians.
They see it as clear US backing for Israeli rule over the whole city, whose eastern part Palestinians lay claim to.
Top US officials, including President Donald Trump's daughter and her husband, are attending Monday's event.
The dedication ceremony is now under way.
Gaza's Islamist rulers, Hamas, have led mass protests in a "Great March of Return" for the past six weeks. Israel says demonstrators are trying to breach the border fence.
Children were among those killed on Monday, the Hamas-run health ministry says.
■ Jerusalem: Trump move prompts negative world reaction
■ Trumplomacy: Key takeaways from Jerusalem policy shift
Palestinians hurled stones and firebombs, while the Israeli military used snipers as black smoke poured from burning tyres.
Israel's army said 35,000 Palestinians were taking part in "violent riots" along the security fence and that its troops were operating "in accordance with standard procedures".
What is going on in Gaza?
Palestinians have held weekly protests there in the run-up to their annual commemoration of what they call the Nakba or Catastrophe, when hundreds of thousands of their people fled their homes or were displaced following the foundation of the Israeli state on 14 May, 1948.
Scores of Palestinians have been killed since the protests began. Thousands more have been wounded.
Hamas, which is in a state of conflict with Israel, had said it would step up protests in the lead-up to Tuesday, the official Nakba commemoration.
It says it wants to draw attention to what Palestinians insist is their right to return to ancestral homes in what became Israel.
"Today is the big day when we will cross the fence and tell Israel and the world we will not accept being occupied forever," a science teacher in Gaza, Ali, told Reuters news agency.
Israel says the protests are aimed at breaching the border, which it guards heavily, and attacking Israeli communities nearby.
The Israeli military said it had killed three people trying to plant explosives near the security fence in Rafah.
It said aircraft had also "targeted Hamas military posts near the Jabalia area after troops were fired upon".
Why is the embassy move so controversial?
The status of Jerusalem goes to the heart of the Israeli-Palestinian conflict.
■ Israel and the Palestinians: Can settlement issue be solved?
■ What are alternatives to a two-state solution?
Israeli sovereignty over Jerusalem is not recognised internationally and, according to the 1993 Israel-Palestinian peace accords, the final status of Jerusalem is meant to be discussed in the latter stages of peace talks.
Israel has occupied East Jerusalem since the 1967 Middle East war. It effectively annexed the sector, though this was not recognised by any countries until Mr Trump's declaration in December 2017.
Since 1967, Israel has built a dozen settlements, home to about 200,000 Jews, in East Jerusalem. These are considered illegal under international law, although Israel disputes this.
Various countries once had embassies based in Jerusalem but many moved after Israel passed a law in 1980 formally making Jerusalem its capital.
■ What makes Jerusalem so holy?
■ Why do evangelicals support Trump on Jerusalem?
President Trump's decision last year to recognise Jerusalem as Israel's capital broke with decades of US neutrality on the issue and put it at odds with most of the international community.
A boost for Netanyahu
By Jeremy Bowen, BBC Middle East editor, Jerusalem
The embassy move is the culmination of one of the best weeks in the political life of Israel's Prime Minister, Benjamin Netanyahu.
First President Trump kept his promise to pull out of the Iran nuclear deal. Now the US embassy is moving.
Placards in Jerusalem praise Mr Trump. The local football club, Beitar, infamous for fans who chant "death to Arabs", has included "Trump" in its name.
The embassy move has been rejected by the main allies of Israel and the US. Palestinians are protesting in their thousands in Gaza.
It is much more low-key in the West Bank, including occupied East Jerusalem.
The embassy move is good for the Netanyahu government, good for President Trump's base and makes most Israelis pleased but there is no evidence to back Mr Netanyahu's claim that it is good for peace.
What will be opened and who will attend?
A small interim embassy will start operating on Monday inside the existing US consulate building in Jerusalem.
A larger site will be found later when the rest of the embassy moves from Tel Aviv.
The opening ceremony was brought forward to coincide with the state of Israel's 70th anniversary.
President Trump is expected to address those attending Monday's event via video link. In a tweet, he said it was "a great day for Israel".
Alongside Ivanka Trump and Jared Kushner, who are both senior White House advisers, Treasury Secretary Steven Mnuchin and Deputy Secretary of State John Sullivan are at the ceremony.
The EU has voiced strong objections to the embassy move.
The decision to recognise Israel as Jerusalem's capital and move the embassy is strongly supported by Israeli Jews across the often fractious political spectrum.
Palestinian Authority President Mahmoud Abbas, however, has described Mr Trump's decision as the "slap of the century". He says the US can no longer be considered a neutral broker in on-off Israeli-Palestinian peace talks and cannot have any future r
 
Tambua Madhara ya Ulaji wa Chipsi

MUUNGWANA BLOG / 17 hours ago



Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree.

Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija

Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini.
Pia inasadikika mafuta yaliyopo katika chipsi katika sahani moja ya chisi ya moto endapo utaamua kuchuja kuna uwezekano wa kupata nusu glasi ya mafuta ya kupikia. Kwa hali hii ujue ni hatari.

Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana tunapokula vyakula vyingi vyenye mafuta mengi hutupelekea kuongeza unene na uzito.

Unene huwa ni chanzo cha magonjwa mengi ,Kwani (High Blood pressure) hutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini ambayo hupelekea mirija ya kusafirisha damu kuwa na mafuta. Hii husababisha njia ya kupitia damu kuwa nyembamba hivyo kusababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini kama inavyotakiwa. Nguvu hii ya ziada huongeza au kupunguza mapigo ya moyo.

Mapigo ya moyo yanapoongezeka sana ni hatari na yanapo pungua sana pia ni hatari.
Hivyo basi ni vizuri kwa watumiaji wa chipsi kujitahidi kutumia kwa kiasi kidogo au kuacha kabisa vile vile mazoezi pia ni muhimu ili kupunguza mrundikano wa mafuta katika mwili.

Pia inasemekana kuwa wanasayansi wamegundua kuwa chipsi husababisha kukuza hips hivyo kwa wanaume wengi hawatapenda kuwa katika hali hiyo, hivyo ni muhimu kujiepusha na pia isije ikawa kichocheo kwa wanawake kutumia sana ili kukuza sehemu hizo za maumbile bali wapunguze kutumia chipsi pamoja na kufanya mazoezi ili kuweka mwili katika hali ya kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.pia ulaji wa chips kupita kiasi husababisha wanaume na wanawake kuzeeka mapema.
Darasa zuri, kuna watu wanasema uzi huu tunajadili pumba, waje wasome makala kama hizi zinazonyofolewa sehemu nyingine ili kuwanufaisha wanauzi huu.
 
Back
Top Bottom