Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mambo ambayo ni sumu katika mahusiano yako ya mapenzi

MUUNGWANA BLOG / 4 days ago



Katika harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi.

Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi.

1. Wivu kupindukia.
Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi.

Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu.

2. Kutompa nafasi mpenzi wako.
Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi.

Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha.

3. Kumuingilia mpenzi katika mambo yako.
Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia.

Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako.
 
Yajue Madhara yatokanayo na Matumizi ya Bangi

MUUNGWANA BLOG / 4 days ago



Kwanza kabisa bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Mmea huu huko mitaani una majina mengi, majina hayo ni kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga.

Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish.

Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe (hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake, nan do maana mtu akitumia bangi mara nyingi hufanya vitui vya ajabu sana.

Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.

Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu, maua, na mche na huwa na rangi ya kijani, kijivu au brauni, lakini bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika sehemu nyingi duniani.

Bangi hutumika kwa kuvuta moshi kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na watumiaji kama “blunt”

Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo katika uhalisia (ndoto za mchana/ maruweruwe). Matokeo haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC kilichovutwa na ukali wake.

Mara nyingi wavutaji wa bangi huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.

Matatizo ya ubongo yanayopelekea kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.

Hivyo kila wakati kwa ulinzi na usalama wa afya epuka matumizi ya bangi.
 
Back
Top Bottom