Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Leonardo Da Vinci (Vinci,Toscana, Italia, 15 Aprili 1452 –Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwamtu mwenye vipaji vingivingi kutoka italy
Kifupi, alikuwa mwanahisabati,mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi,mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji,msanifu majengo, mwanabotania,mwanamuziki na mwandishi.
Ndiye mwakilishi bora wa tapo laRenaissance.
 
Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.
Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa nashauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".
 
Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.
Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli,kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuzanishati ya jua kuwa umeme.
 
Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani niMona Lisa na Karamu ya mwisho.
 
Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili1452, mkoani Toscana, katika mji mdogo wa kilimani wa Vinci, katika mabonde ya Mto Arno, karibu naFlorence nchini Italia.
Babu yake, Ser Antonio, anajivunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwahawajaoana. Baba yake alikuwamwanasheria, Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci. Mama yake, Caterina, alikuwa mhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutokaMashariki ya Kati.
 
. Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa Bwana Piero kutoka Vinci".
Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba yashambani na mama yake. Halafu akaja kuishi Vinci na baba yake, mkewa baba yake aliyeitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco.
 
Back
Top Bottom