Mama yake akaelekea London na watoto wote, ambako alikua akiendelea na masomo katika chuo cha Staffort. Mwaka 1968, Sanchez akiwa na miaka 19 alichukuliwa na babake akasome Paris, Ufaransa, lakini Sanchez aligoma kabisa na kupendekeza apelekwe chuo kikuu cha Patrice Lumumba kilichopo Moscow mji mkuu wa Urusi. Kwa mujibu wa BBC, chuo hiki kiliasisiwa kwa malengo ya kuandaa viongozi wenye misimamo mikali ya kikomunisti hasa wa nchi za dunia ya tatu. Chuo hiki kimepika viongozi wa juu wa nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Sudan, Namibia, Benin, Afrika ya kati nk.
Kutokana na tabia za ukorofi, fujo, utukutu, uhuni na kuishi kiPlayboy alichukiwa sana na wakufunzi. Mwaka 1969 Sanchez aliandaa maandamano ya wanafunzi wa kiarabu nchini hapo, kosa lililomfukuzisha chuoni hapo.