Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati Dk Kaganda anasema hayo, wataalamu wa afya nao wanasema ugonjwa wa kupasuka midomo mara nyingi husababishwa na midomo kupigwa na miale ya jua, baridi na upepo mkali pamoja na kukosekana kwa vitamini kadhaa mwilini, matumizi ya dawa mbalimbali, msongo wa mawazo na maradhi ya kinywa.
 
Baadhi ya dawa za meno wataalamu hao wamezitaja kuwa nazo huchangia midomo kupasuka kwasababu baada ya kusugua meno, midomo hukakuka kutokana na dawa hizo kuwa na sodium salfeti ambayo husababisha ngozi kukauka na hata kuwasha.

Pia wanasema matunda yenye aside nyingi kama ya jamii ya machungwa, nayo pia huchangia midomo kukauka.
 
Lakini Dk kaganda anaeleza sababu nyingine kuwa mgonjwa mwenye homa kali, naye yuko hatarini kupasuka midomo yake.

“Sababu nyingine ni ya mtu anayeharisha sana na kusababisha kupungukiwa na maji, hivyo ngozi huanza kukauka na midomo yake eneo la pembeni inaweza kupasuka na hata maambukizi ya virusi nayo huchangia mtu kukumbwa na tatizo la kupasuka midomo,” anasema Dk huyo.
 
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, zipo dalili za moja kwa moja za kuashiria mtu kupatwa na tatizo hilo ambazo ni pamoja na midomo kuvimba, kuweka malengelenge, midomo kuwa mikavu na yenye rangi nyekundu.

Wakati mwingine ngozi ya midomo hujimenya na kusababisha iwashe na muathirika hupata maumivu makali, jambo ambalo linasababisha midomo ianze kutoa damu.
 
♡
Screenshot_20180511-221321.jpg
 
Tiba ya ugonjwa huo ni ipi?

Kila ugonjwa huwa na tiba yake kwa lengo la kuutuliza au kuumaliza kabisa.

Dk Kaganda anasema tiba ya awali isiyo na gharama kwa muathirika ni pamoja na kutumia chakula chenye vitamin C na E.

“Tiba ya mapema ambayo haimgharimu mtu ni ya kutumia mboga za Majani, matunda na atumie tiba lishe ya Vitamini C au atumie mafuta ya vaselini kwa kuipaka midomo yake ili isikauke sana, kwani ikikauka sana itamsababishia maumivu zaidi,” anasema Dk huyo.
 
Lakini kama mgonjwa atakuwa amepungukiwa na maji mwilini, kuna njia mbadala ya kumsaidia ambayo ni ya kumuongezea maji na kama itakuwa imepasuka kupita kiasi huchomwa sindano.

Inaelezwa kuwa hatua nyingine ya kutibu tatizo hilo ni pamoja na kunywa maji mara kwa mara na kama muathirika atakuwa anaupungufu wa maji, ataongezewa na wakati mwingine madaktari humfanyia uchunguzi wa kina ili kuhakikisha tatizo hilo linamalizika.
 
Inashauriwa mtu kujipaka mafuta maalumu ya midomo ya kujikinga na jua kama mtu unatoka nje kwenye mazingira ya jua kali au baridi na upepo mkali, kunywa vitu vingi vyenye majimaji, kupaka mafuta ya midomo hasa yenye vitamin E na Alovera, hiyo ni njia nzuri ya kuzuia midomo kupasuka.

Mtu anashauriwa kutumia mafuta maalumu ya midomo iliyowekwa radha mbalimbali za matunda ambazo humshawishi kujilamba midomo yake kila mara.
 
Madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na kuwa na midomo iliyokauka ni pamoja na mgonjwa kuugua kwa muda mrefu na wakati mwingine ugonjwa huo unaweza kumrudia mara kwa mara kutokana na ngozi yake kuwa kavu kwa muda mrefu kutokana na ngozi ya mwili nayo kuwa kavu kwa muda mrefu kwasababu ya kukosa homoni ya tezi.
 
Back
Top Bottom