Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

376ab470-b1ec-4852-aa14-02dae7beb835.jpg
 
Mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni shahidi wa nane wa utetezi, Muslim Mmbaga (35), jana aliwaacha hoi wasikilizaji katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, alipodai mtu anayedaiwa kumuua, yuko mitaani anatembea.

Mmbaga ambaye aliitwa kumtetea mshtakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed, alidai marehemu Sebari Kitivo Mbura ni shahidi wa mashtaka katika kesi ya bilionea Erasto Msuya.
 
Hivi unajua kuwa maziwa ya mama ni muhimu kwa afya na makuzi ya mtoto katika miezi sita ya kwanza?

Ukweli ni kwamba kila mama anasimulizi yake ya namna anavyomnyonyesha au kutomnyonyesha mwanawe.

Wapo wanaokacha kuwanyonyesha watoto wao wakihofia kuharibu maumbile ya matiti yao lakini wengine wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya maradhi au kutingwa na kazi hasa za kujiongezea kipato.
 
Utafiti mpya wa Shirika la Afya Duniani (Unicef) unaonyesha takribani watoto 7.6 milioni duniani hawanyonyeshwi kila mwaka.

Utafiti huo unaonyesha idadi ya watoto wasio nyonyeshwa na mama zao ni kubwa zaidi katika mataifa yaliyoendelea ikilinganishwa na yale maskini.

Asilimia nne ya watoto kwenye nchi maskini hawanyonyeshwi kabisa maziwa ya mama wakati katika nchi zilizo endelea ni asilimia 22.
 
Viwango vya unyonyeshaji vilivyofanyiwa tathimini mwaka jana na Unicef kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika nchi 194 ilibaini asilimia 40 tu ya watoto walio chini ya miezi sita wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee.

Pia, ni nchi 23 pekee duniani ndizo zenye kiwango cha unyonyeshaji wa zaidi ya asimilia 60.

Ofisa Mawasiliano wa Unicef Tanzania, Usia Nkoma anasema wametoa utafiti huo na kutoa matokeo yake mwezi huu kuikumbusha dunia umuhimu wa kunyonyesha watoto.
 
Kila mtoto hai anasherehekea siku ya mama duniani kwa hiyo ni jukumu la akina mama kutimiza wajibu wao wa msingi wa kuwanyonyesha watoto wao kwa sababu maziwa ya mama ndiyo msingi bora wa maisha yake,” anasema.

Nkoma anasema jamii inao wajibu mkubwa wa kuhakikisha mama anapata nafasi ya kumnyonyesha mtoto wake bila wasiwasi wowote.

Hivi karibuni, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliwaonya watumishi wasio toa nafasi kwa akina mama wenye watoto kuwahi kutoka ofisini na kwenda kunyonyesha.
 
Serikali ya awamu ya tano, katika kuhakikisha watoto wanakuwa na afya bora imeweka kanuni inayompa nafasi ya saa mbili mama mwenye mtoto wa chini ya miezi sita kumnyonyesha mwanawe,” anasema Ummy.

Simulizi za unyonyeshaji

Katika jamii wapo kina mama wanaonyonyesha watoto wao kwa miezi sita, mwaka mmoja na wengine miwili.
 
Lakini pia wapo wasiopenda kabisa kunyonyesha kwa sababu mbalimbali.

“Nilikuwa nabanwa sana na kazi ikabidi nimuanzishie mtoto wangu maziwa ya kopo akiwa na miezi minne, ndiyo muda niliomuachisha,” anasema Anitha Linus (jina la pili sio sahihi).

Anitha anajipa moyo kuwa japo alimuachisha mwanawe katika umri huo alihakikisha anampatia maziwa hayo na mpaka sasa anamiaka miwili.
 
Adelina Elias anasema mwanawe wa mwezi mmoja hanyonyi baada ya kupata maradhi ya kuvimba matiti.

“Nilijitahidi kutibiwa lakini maumivu makali na uvimbe vimemfanya mwanangu asinyonye na sasa nampatia uji ambao unga wake umechujwa,” anasema Adelina. Anasema kama atatibiwa na kumaliza tatizo hilo, bado uwezekano wa kumnyonyesha tena hautakuwapo tena kwa sababu maziwa yatakuwa yameshakauka.

Wakati kina mama hao wakiyasema hayo, Ofisa Mawasiliano wa Unicef Nkoma anasema sio tu kumfanya mtoto akue ipasavyo, unyonyeshaji unamuwezesha kuwa na upeo mkubwa kiakili jambo ambalo pia ni sifa kwa mama.
 
Adelina Elias anasema mwanawe wa mwezi mmoja hanyonyi baada ya kupata maradhi ya kuvimba matiti.

“Nilijitahidi kutibiwa lakini maumivu makali na uvimbe vimemfanya mwanangu asinyonye na sasa nampatia uji ambao unga wake umechujwa,” anasema Adelina. Anasema kama atatibiwa na kumaliza tatizo hilo, bado uwezekano wa kumnyonyesha tena hautakuwapo tena kwa sababu maziwa yatakuwa yameshakauka.

Wakati kina mama hao wakiyasema hayo, Ofisa Mawasiliano wa Unicef Nkoma anasema sio tu kumfanya mtoto akue ipasavyo, unyonyeshaji unamuwezesha kuwa na upeo mkubwa kiakili jambo ambalo pia ni sifa kwa mama.
 
Naye Kaduma anasema kihalisia, mtoto mchanga anatabia ya kulala usingizi ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa.

“Katika muda huo anapaswa kunyonyeshwa, kwa hiyo mama usione uvivu wala maumivu kumnyonyesha titi lako mtoto baada ya kuzaliwa,” anasema.

Anasema kihalisia mtoto hatakuwa na hamu ya kunyonya ndani ya muda huo hivyo ni jukumu la mama kumshawishi ili anyonye.
 
Back
Top Bottom