Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Screenshot_20180514-100537.jpg
 
Sokratis Papastathopoulos

Umri: Miaka 29

Klabu inayomtaka: Arsenal

Staa huyo wa kimataifa wa Ugiriki amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake Borussia Dortmund. Mkuu wa Idara ya Usajili ya Arsenal, Sven Mislintat, ndiye aliyefanya usajili wa mchezaji huyo alipomtoa Werder Bremen kumpeleka Dortmund miaka mitano iliyopita.

Papastathopoulos alishawaambia waajiri wake Dortmund kwamba hatasaini mkataba mpya kwenye timu hiyo na kuifanya Arsenal kuonyesha dhamira ya dhati kabisa kumsajili hasa kwa kipindi hiki ukizingatia Mislintat yupo kwenye kikosi hicho cha wababe wa Emirates.
 
Wilfried Zaha

Umri: Miaka 25

Klabu inayomtaka: Tottenham

Ripoti za karibuni zinafichua kwamba Manchester City inahitaji huduma ya winga huyo wa Crystal Palace, lakini Tottenham Hotspur ni miongoni mwa timu zinazomhitaji mchezaji huyo ambaye msimu huu amekuwa na kiwango bora kabisa.

Soka la Zaha liliisaidia timu hiyo kukwepa kushuka daraja huku akijitengenezea jina kwa kiasi kikubwa na kufanya timu vigogo kwenye Ligi Kuu England kupigana kuwania huduma yake.
 
Palace itambana kumbakiza, lakini ukweli ni kwamba itakuwa kwenye vita itakayowashinda uwezo kwa sababu mchezaji yeyote atahitaji kwenda kwenye timu ambayo itampa changamoto za kukua zaidi na hilo hawezi kulipata huku Palace.
 
Aaron Ramsey

Umri: Miaka 27

Klabu inayomtaka: Chelsea

Kuna wakati Manchester United iliingia kwenye mpango wa kumnasa kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey.

Kiungo huyo alikuwa kipenzi cha Arsene Wenger, ambaye msimu ujao hatakuwapo kwenye timu hiyo. Ripoti zinafichua kwamba Arsenal inataka kumpiga bei kwenye dirisha lijalo na sasa Barcelona na Chelsea zinapiga hesabu za kuinasa huduma yake.

Mkataba wa Ramsey umebakiza miaka miwili kufika tamati na haonekani kutaka kusaini dili jipya.
 
Back
Top Bottom