Mbona hakuna kitu bro. Unaweza kuyasoma haya mambo kwenye Google tu...
Einstein alikuwa mtu wa aina yake sana. Mpaka leo watu wa conspiracy theories wanadai eti ama alitoka masayari mengine huko au alikuwa anaoteshwa hizi siri na aliens. Mwaka 1905 unajulikana kuwa ni Mwaka wa Miujiza katika ulimwengu wa Sayansi kwa sababu mwaka huo Einstein, akiwa karani wa kawaida katika idara ya Hatimiliki, alichapisha pepa tatu zilizobadilisha kabisa mwelekeo wa sayansi na kufunua siri nyingi za kiumbaji. Pepa hizi ndizo zilimaliza monopoly ya mawazo ya Isack Newton na kuiingiza dunia katika mkondo mpya. Pepa moja ndiyo iliweka misingi ya nadharia yake mashuhuri ya General Relativity (uhusiano wa space na time). Nyingine ikaelezea asili ya mwanga (hii ndiyo ilikuja kumpatia Zawadi ya Nobel katika Fizikia baadaye). Pepa ya tatu nadhani ndiyo iliweka misingi ya fomyula mashuhuri kuliko zote duniani E = MC2. Ajabu ni kwamba jamaa wala alikuwa hafanyi majaribio yo yote kama ilivyo kawaida ya wanasayansi wengine. Yeye alikuwa na kawaida ya kufanyia majaribio yake kichwani tu kwa kupitia nguvu za kuwaza. Mpaka leo hii sayansi yote inahangaika kuboresha nadharia zake na kuona jinsi zinavyoweza kutusaidia katika maisha ya kawaida. Leo hii vitu kama microwave, lasers, rada, microchip na hata mawazo tata katika science fiction kama time machines, wormhole, black holes na mengine mengi yanawezekana kutokana na utabiri uliomo katika mojawapo ya nadharia zake angavu.