Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_20180521_183758_724.jpg
 
Kikosi kamili cha Uhispania
Walinda lango: David de Gea (Manchester United), Pepe Reina (Napoli), Kepa Arrizabalaga (Athletic Bilbao).
Mabeki: Jordi Alba (Barcelona), Nacho Monreal (Arsenal), Alvaro Odriozola (Real Sociedad), Nacho Fernandez (Real Madrid), Dani Carvajal (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Cesar Azpilicueta (Chelsea).
Kiungo wa kati: Sergio Busquets (Barcelona), Isco (Real Madrid), Thiago Alcantara (Bayern Munich), David Silva (Manchester City), Andres Iniesta (Barcelona), Saul Niguez (Atletico Madrid), Koke (Atletico Madrid).
Washambuliaji: Marco Asensio (Real Madrid), Iago Aspas (Celta Vigo), Diego Costa (Atletico Madrid), Rodrigo Moreno (Valencia), Lucas Vazquez (Real Madrid).
 
Kisiwa kimoja nchini Brazil ambapo ni marufuku kwa mwanamke kujifungua kinasherehekea mtoto wa kwanza kuzaliwa humo katika kipindi cha miaka 12.
Kisiwa cha Fernando de Noronha kinachopatikana 370km (maili 230) kutoka mjini Natal, kina wakazi takriban 3,000 lakini hakika hospitali za kujifungulia waja wazito.
Wanawake wanaotaka kujifungua hutakiwa kusafiri bara.
Mwanamke ambaye hakutaja jina lake litajwe alijaliwa msichana Jumamosi kisiwani humo.
 
Anasema hakufahamu kwamba alikuwa mja mzito na kwamba alipigwa na butwaa.
Mshangao
Mwanamke huyo anaaminika kuwa na miaka 22.
"Ijumaa usiku nilianza kuhisi maumivu na nilipokwenda kwenye bafu nitagundua kitu kikitoka kupitia miguu yangu," amenukuliwa na tovuti ya O Globo.
"Ni wakati huo ambapo babake mtoto alifika na kumchukua mtoto huyo. Alikuwa mtoto, msichana. Nilipigwa na butwaa."
Mtoto huyo alichukuliwa na kupelekwa hospitalini baadaye.
 
Maafisa wa serikali eneo hilo wamethibitisha kisa hicho.
"Mamake mtoto, ambaye hataki jina lake lifichuliwe, alianza kupatwa na uchungu wa kuzaa akiwa nyumbani," taarifa ya serikali inasema, kwa mujibu wa O Globo.
"Familia hiyo inasema haikufahamu kuhusu mimba ya mwanamke huyo."
Ili kusherehekea kisa hicho nadra cha kuzaliwa kwa mtoto kisiwani, wakazi wanaisaidia familia hiyo, na kuwapa nguo za kuvaliwa na mtoto huyo, ripoti zinasema.
 
Fernando de Noronha ni kisiwa ambacho kina baadhi ya fukwe maridadi zaidi duniani na ni maarufu kwa hifadhi ya viumbe wa baharini.
Kisiwa hicho hupatikana eneo la hifadhi ya bahari na idadi ya watu imekuwa ikidhibitiwa kwa muda kisiwani humo.
 
Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata ameachwa nje ya kikosi cha wachezaji 23 watakaowakilisha Uhispania katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.
Mchezaji huyo wa miaka 25 alifunga mabao 11 msimu wake wa kwanza Stamford Bridge na alichezeshwa kama nguvu mpya dakika za mwisho mwisho wakati wa fainali ya Kombe la FA ambapo Blues walilaza Manchester United 1-0 Jumamosi.
Wachezaji wenzake Morata katika Chelsea Marcos Alonso na Cesc Fabregas wanaungana na beki wa Arsenal Hector Bellerin katika kuachwa nje ya kikosi.
Mtangulizi wa Morata katika Chelsea Diego Costa ni miongoni mwa washambuliaji watakaoelekea Urusi.
 
Julen Lopetegui amewaweka wachezaji wanne wa Ligi ya Premia kwenye kikosi chake: David De Gea, David Silva, Cesar Azpilicueta na Nacho Monreal.
Uhispania wataanza kampeni yao Urusi kwa mechi dhidi ya Ureno mnamo 15 Juni mjini Sochi.
Morata aliwachezea mabingwa hao wa dunia wa 2010 mara ya mwisho Novemba 2017 alipofunga katika mechi ambayo walishinda 5-0 dhidi ya Costa Rica.
Licha ya kuachwa nje ya kikosi, mshambuliaji huyo ameandika kwenye Twitter ujumbe wa kuwapongeza na kuwatakia heri wenzake katika michuano hiyo.
 
Back
Top Bottom