'Mpumbavu akitajirika hakai na wenzake'
Panya mmoja alimeza almasi ya tajiri, yule tajiri alipogundua akatafuta mtu ambaye ni muua panya ili aipate almasi yake.
Muua panya alipofika kwa tajari, alionyeshwa dari wanapojificha panya wengi.
Muua panga alipoingia darini akakuta panya wengi sana wamekusanyika pamoja, lakini panya mmoja peke yake alikaa pembeni.
Papo hapo akamuu yule panya na alipompasua ndani kweli akakuta almasi ya tajiri.
Tajiri kwa mshangao huku akiwa haamini, akamuuliza muua panya kuwa umemjuaje kwa haraka vile panya mwenye almasi yake wakati kuna panya wengi.
Yule kijana muua panya akamjibu tu 'MPUMBAVU AKITAJIRIKA HAKAI NA WENZAKE'