Magonjwa yasiyoambukiza (Non Communicable Diseases)
Magonjwa haya kwa kifupi huitwa ‘NCD’s’. Haya ni magonjwa sugu ambayo humuathiri mtu kwa kipindi kirefu na kadiri siku zinavyoendelea na ugonjwa huendelea mwilini taratibu.
Wakati mwingine magonjwa haya yasiyoambukiza husababisha vifo mapema na kwa haraka yaani tangu mtu anapoanza kuugua kabla hajakamilisha vipimo au dozi aliyopangiwa hufariki.
Baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza ni kama vile matatizo ya mfumo wa kinga mwilini ambayo ni magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa au saratani, kisukari, magonjwa sugu ya figo, magonjwa ya mifupa, kupoteza kumbukumbu na kutetemeka mwili ambalo ni tatizo la ubongo na huwapata wazee, magonjwa yanayopunguza uwezo wa macho na mengine mengi.