Si hivyo tu, ni haki ya mbwa kupewa mazoezi ya viungo na kuvalishwa nguo pindi baridi inapozidi. Ni lazima na ni haki ya mnyama huyo kupewa tiba pindi anapoumwa au kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa mwili, Wazungu wanaita, “checkup” mara kadhaa kwa mwaka. Si hilo tu, pia anakatwa kodi.
Supermarket pia zimejaa vyakula maalumu vya mbwa, kuna saluni maalumu za mbwa na kuna viwanja maalumu vya michezo ya mbwa.
Jonas Kater, raia wa Ujerumani mkazi wa Koln, ni miongoni mwa wanaopenda mbwa. Anasema mbwa kwa mila za Ujerumani ni kiumbe wa familia au kwa maneno mengine ni mwanafamilia.