Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kula matunda na mbogamboga kwa wingi
Vyakula hivi husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini, hivyo kujikinga na maradhi mbalimbali. Vyakula hivi pia huupatia mwili makapi-mlo ambayo humfanya mtu ajisikie kushiba na kumfanya ale chakula kwa kiasi kidogo hivyo kupunguza uwezekano wa kuwa na uzito uliozidi au unene.
Safi kabisa
 
Kula vyakula vyenye makapi-mlo kwa wingi
Makapi-mlo husaidia mfumo wa chakula kufanya kazi kwa ufanisi. Pia husaidia mtu kupata haja kubwa kwa urahisi na huchangia katika kupunguza uwezekano wa kuongezeka uzito, kupata baadhi ya saratani, magonjwa ya moyo na kisukari.
Ongeza kiasi cha makapi-mlo kwa kula matunda na mbogamboga kwa wingi, nafaka zisizo kobolewa kama unga wa dona na ngano na vyakula vya jamii ya kunde
Safi sana mkuu
 
Epuka vyakula vyenye mafuta mengi
Mafuta hutoa nishati lishe kwa wingi hivyo husababisha ongezeko la uzito kwa haraka. Ulaji wa mafuta mengi hususani yenye asili ya wanyama huchangia katika kuongeza kiasi cha mafuta katika damu hususani lehemu na hivyo kuongeza uwezekano wa kupata maradhi sugu kama magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo kubwa la damu.
Sawa kiongozi, ubarikiwe
 
Epuka kutumia sukari nyingi
Sukari huongeza nishati-lishe bila virutubishi vingine mwilini. Punguza kiasi cha sukari kwa kuepuka vinywaji vyenye sukari nyingi na kunywa juisi halisi ya matunda, togwa au vinywaji vya viungo. Epuka vyakula vyenye sukari nyingi kama vile jamu, biskuti, keki, chokoleti, kashata na pipi.
Sawa
 
Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi
Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi huongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu na baadhi ya saratani. Matumizi ya chumvi huweza kupunguzwa kwa kutumia chumvi kidogo wakati wa kupika, kuepuka vyakula vyenye chumvi nyingi au vilivyosindikwa kwa chumvi. EPuka tabia ya kuongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula (mezani).
Vema mkuu
 
.
Wallpaper.jpg
 
Kunywa maji safi, salama na ya kutosha
Inashauriwa kunywa maji angalau glasi nane(lita moja na nusu) kwa siku. Maji ni muhimu sana mwilini kwani:
  • hurekebisha joto la mwili,
  • husaidia uyeyushaji wa chakula,
  • husafirisha virutubishi kwenda kwenye seli na kuondoa mabaki au uchafu mwilini kwa njia ya jasho, mkojo nk.
  • Husaidia pia kulainisha maungio ya mwili.
Sawa kabisa
 
Back
Top Bottom