Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tafiti zimeonyesha, kuna uhusiano kati ya ulishaji wa mtoto na uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza utotoni, katika ujana na hata anapokua mtu mzima. Unyonyeshaji wa maziwa ya mama huwakinga watoto dhidi ya kuwa na uzito uliozidi na unene uliokithiri hapo baadaye
 
Watoto walionyonyeshwa maziwa ya mama kwa muda mfupi(chini ya miezi 6) na wale waliopewa maziwa mbadala (ya kopo au wanyama) wako katika hatari zaidi ya kupata baadhi ya magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo kubwa la damu na saratani utotoni, katika ujana na wanapokua watu wazima.
 
Ulishaji mtoto vyakula vya nyongeza vyenye nishati-lishe kwa wingi unahusishwa na mtoto kuwa na hatari ya kupata saratani na shinikizo kubwa la damu ukubwani
Unene wakati wa utoto humweka mtoto katika hatari ya kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama kisukari na ugonjwa wa moyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…