Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

852734525_232236.jpg
 
Baada ya Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017/18, itaondoka na donge nono la takribani Sh227 bilioni.
Awali, Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) lilitangaza zawadi ya bingwa wa mashindano hayo msimu wa 2017/18 atajizolea Euro 100 milioni ambayo ni sawa na takriabani Shilingi 227 bilioni.
Msimu uliopita, Real Madrid ilinyakua taji hilo baada ya kuichapa Juventus kwenye mchezo wake wa fainali na kutetea taji hilo.
Katika fainali hiyo ya mwaka 2017 Real Madrid walivuta mkwanja wa Euro 89.5 milioni.
Mashindano hayo ndiyo yanatajwa kuzipa timu kiasi kikubwa cha pesa ukilinganishwa na mashindano yoyoye yale duniani ya soka.
 
Baada ya Nyota wa Liverpool kupelekwa hospitalini na kufanyiwa vipimo vya awali X-Ray ili kubaini ukubwa wa tatizo lililomkabili, taarifa inaeleza kwamba mchezaji huyo hajapata majeraha makubwa na anaweza kupona haraka kabla ya kuanza fainali za Kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Misri inaeleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha hali yake sio mbaya sana.
Chama hicho cha soka cha Misri kilitoa taarifa yake jana baada ya fainali hiyo kuisha ikieleza kwamba, daktari wa timu hiyo amewaeleza maofisa wa afya ya Liverpool kuwa wanaamini Salah hasumbuliwi na tatizo kubwa na atakiwa kufikiria kuwa atacheza Kombe la Dunia.
 
Mashabiki mbalimbali wa soka duniani wamekuwa wakituma salamu zao za pole kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Twitter wakimuombenyota Salah apone haraka baada ya kupata majeraha kwenye mchezo fainali dhidi ya Real Madrid wa jana Jumamosi usiku.
Mo Salah aliangusha chozi akiwa uwanjani baada ya kupata majeraha begani kisha kutoka uwanjani katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza.
Mo Salah alipoteza mwelekeo baada ya kupigana vikumbo na Sergio Ramos jambo lililosababisha kukita chini na kuumia bega.
 
KILA kona ya dunia, kabla ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kati ya Real Madrid na Liverpool mashabiki wa soka walikuwa wanataka kuona mpambano wa Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah.
Kila mmoja alikuwa akisema yake, ukali wa mchezaji lakini hali ilikuwa tofauti, kabla ya hata mchuano haujakolea vizuri, beki wa Real Madrid, Sergio Ramos akakatisha matamanio ya watu.
 
Alitumia dakika 30 kufuta kilichokuwa kikifikiriwa na wengi. Alimuumiza Salah, lakini akajaribu kuendelea na mchezo ikashindikana akatoka huku akimwaga machozi.
Chozi la Salah liko katika pande mbili, kuikosa fainali ya Ulaya na kushindwa kufanya kile alichokuwa anakiwaza lakini kikubwa ni kuzikosa Fainali za Kombe la Dunia.
Hali hiyo imemfanya Ramos kupingwa kila kona hasa mashabiki wa Liverpool kwa kitendo chake cha kumchezea rafu mbaya na wakati Salah alipokuwa anatolewa nje, alikuwa akicheka tu.
 
Nyota huyo wa Misri alilazimika kutoka dakika ya 31 baada ya kuumizwa na Ramos kwani aliukamata mkono wa Salah na kumsababisha aanguke vibaya kiasi cha kufiukia bega.
Salah alikuwa akilia wakati anatolewa akiwaza ndoto yake kucheza Kombe la Dunia haipo tena. Wakati hali ikiwa hivyo, televisheni zilimnasa Ramos alikuwa akicheka na kutabasamu akiwa na mwamuzi msaidizi akiw apembeni ya uwanja.
 
Ramos ni beki mzuri lakini kile alichokifanya si cha kiuanamichezo,” alisema mchezaji wa zamani, Gary Lineker wakati akiangalia televisheni ya BT Sport.
Wakati hali ikiwa hivyo, Ramos alituma salamu kwa Mohamed Salah akimpa pole lakini alisema kuwa haikuwa nia yake kumuumiza winga huyo wa Liverpool.
Kuumia kwa Salah ni baada ya beki huyo kumvuta mkono walipokuwa wakiwania mpira na kuanguka Ramos.
Bosi wa Liverpool, Jurgen Klopp alifananisha kitendo cha Ramos hadi kumuumiza mchezaji wake ni sawa na mieleka.
 
Back
Top Bottom