Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NDIYO hivyo, Real Madrid wamebeba tena taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya usiku wa jana Jumamosi, kilainii wakajipigia Liverpool 3-1 katika fainali iliyofanyika mjini Kiev, Ukraine.

Liverpool hawatamsahau Gareth Bale, aliyetokea benchi na kuja kupiga mabao mawili matata kabisa, la kwanza la tick-tack, la pili la umbali wa ‘hapa na Mbagala’ unaambiwa. Kwenye fainali hiyo kama kuna mtu alikuwa na usiku mbaya, basi ni kipa wa Majogoo wa Anfield, Loris Karius, ambaye alitoa zawadi ya bao la kwanza, lililofungwa na Karim Benzema na lile la tatu, ambalo alijaribu kudaka shuti la Bale, ambalo lilipigwa kisawasawa. Liverpool wao walipata bao lao la kujifariji kupitia kwa Sadio Mane, lakini kwa fainali hiyo ya usiku wa jana, mabao yote yalipigwa kipindi cha pili, huku Real Madrid wakiweka rekodi ya kubeba ubingwa wa Ulaya kwa misimu mitatu mfululizo, huku ikiwa mara yao ya 13 katika historia.
 
Ilikuwa fainali ya wanaume na wavulana baada ya kuonekana wazi kabisa, Liverpool ilikosa uzoefu mbele ya wapinzani wao, ambao karibu mastaa wake wote walikuwa wamecheza mechi zaidi ya moja za fainali ya michuano hiyo ya Ulaya. Hali mbaya kwa Liverpool ilianzia pale supastaa wao, Mohamed Salah alipoumia bega kwenye kipindi cha kwanza baada ya kupigana vikumbo na Sergio Ramos na baada ya tukio hilo, kila kitu kilibadilika na Los Blancos walianza kutawala mchezo, huku mabeki wa kocha Zinedine Zidane wakicheza kwa kujiachia kabisa. Ukweli ni kwamba haikuwa mechi ngumu kwa Real Madrid, wakimiliki mpira kwa asilimia 61, huku mashuti yao sita yakilenga goli, wakati Liverpool walipiga mashuti mawili tu.
 
Kwenye mechi hiyo, wachezaji wawili waligongesha mwamba, Isco kwa upande wa Real Madrid na Mane kwa vijana wa Jurgen Klopp, ambaye kabla ya mechi hiyo alidai kwamba, hawezi kuwakubali Madrid kama ni timu bora kwa sababu walikuwa bado hawajacheza na timu yake ya Liverpool. Lakini, nadhani kwa sasa akiulizwa swali la kuhusu ubora wa Madrid, atakuwa na majibu yaliyosahihi.
 
446329532_120865.jpg
 
Zidane sasa anaingia kwenye rekodi za kipekee kabisa, akiipa Real Madrid ubingwa wa Ulaya, akautetea na sasa amebeba tena kwa mara ya tatu mfululizo, akiwafanya wababe hao kuandika historia ya kipekee kwenye michuano hiyo yenye hadhi kubwa kwa ngazi ya klabu huko barani Ulaya.
 
Ticha: nani kafunga?
Wanafunzi: Benzemaa
Ticha: aliye assist?
Wanafunzi: kipaaaaaa
Ticha: nani kafunga?
Wanafunzi: Baleeeee
Ticha: aliye assist?
Wanafunzi:kipaaaaa
Ticha:mani of the mechi?
Wanafunzi: Ramosiiiiiii
Ticha: mmetishaaa
Wanafunzi: kama kipaaaaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom