REKODI AMBAZO MPAKA SASA HAZIJAWAHI KUVUNJWA KATIKA SOKA NI PAMOJA NA:
Idadi KUBWA ya mashabiki wengi wa soka kuingia uwanjani:
Hii ni rekodi iliwekwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Uruguay katika dimba la Maracanazo, mchezo huu wa fainali ulitajwa kuingiza idadi rasmi ya watu Laki moja na sabini na tatu elfu mia nane hamsini (173,850) ila inatajwa huenda kuwa idadi hiyo ilivuka na kufikia hadi watu (2,10.000) pamoja na watazamaji wasiokuwa na tiketi.