Bujumbura, Burundi. Punda 10 walionunuliwa na Ufaransa kutoka Tanzania na wakatolewa kama zawadi katika kiijiji kimoja hapa nchini wameibua mjadala hadi kufikia kusema zawadi hiyo ni ‘matusi kwa taifa’.
Haraka Wizara ya Kilimo ikaamuru kuwaweka chini ya karantini punda hao hali iliyozua mjadala kuhusu ujumbe uliomo katika zawadi hiyo.
Punda hao, walionunuliwa kutoka Tanzania kutokana na fedha za mfuko wa misaada wa Ufaransa walitolewa kama zawadi kwa wakazi wa kijiji cha mkoa wa Gitega ikiwa ni mradi uliobuniwa na shirika lisilo la kiserikali kuwasaidia wanawake na watoto kusafirisha mazao ya kilimo, maji, kuni na mizigo mingine.