Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bujumbura, Burundi. Punda 10 walionunuliwa na Ufaransa kutoka Tanzania na wakatolewa kama zawadi katika kiijiji kimoja hapa nchini wameibua mjadala hadi kufikia kusema zawadi hiyo ni ‘matusi kwa taifa’.

Haraka Wizara ya Kilimo ikaamuru kuwaweka chini ya karantini punda hao hali iliyozua mjadala kuhusu ujumbe uliomo katika zawadi hiyo.

Punda hao, walionunuliwa kutoka Tanzania kutokana na fedha za mfuko wa misaada wa Ufaransa walitolewa kama zawadi kwa wakazi wa kijiji cha mkoa wa Gitega ikiwa ni mradi uliobuniwa na shirika lisilo la kiserikali kuwasaidia wanawake na watoto kusafirisha mazao ya kilimo, maji, kuni na mizigo mingine.
 
Mshauri wa rais ameuelezea mradi huo kuwa sawa na “matusi kwa taifa.”

Msemaji wa Rais wa Seneti, Gabby Bugaga aliandika katika Twitter akisema Ufaransa “inatuchukulia sisi kama punda”.

“Kuweni wakweli, je, punda anachukuliwa kuwa alama ya ubora au ni kasoro?” Aliandika.
 
Burundi yakamata punda wote

Jumapili, Waziri wa Kilimo, Deo Guide Rurema alimwagiza kiongozi wa serikali katika eneo hilo kusaidia haraka kuondolewa punda wote ambao wameshagawiwa bila kujali mchakato wa kiufundi uliofikiwa katika kugawa wanyama hao kutoka nje.

Alhamisi iliyopita, siku ambayo mradi huo ulizinduliwa, Balozi wa Ufaransa Laurent Delahousse alipongeza “uzinduzi wa Land Cruiser aina ya wanyama Burundi”.

Baada ya kuibuka utata huo balozi huyo alisema kwa uelewa wake ‘taratibu zote zilifuatwa.’

Ubelgiji imewahi kuzindua miradi kama hiyo katika mkoa wa Ryigi lakini haikuwa na tatizo lolote.
 
Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyohusisha pikipiki na basi mali ya kampuni ya Saratoga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo limetokea leo, Mei 29 saa 6 mchana katika eneo la kituo cha mafuta cha Munio, mjini hapa.

Amewataja wanafamilia Marehemu hao ni wakazi wa kitongoji cha Katandala mjini hapa.

Kamanda Kyando amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Saratoga lenye namba T 211 AED aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Ally Fabiano (31) mkazi wa Kigoma.

“Basi hilo lilikuwa likitokea Sumbawanga mjini kuelekea mkoani Kigoma,” amesema

Kyando amesema kuwa wanafamilia hao walikuwa wamepanda pikipiki yao iliyokuwa ikiendeshwa na Senga.

"Ilikuwa vigumu hata kuitambua miili ya wale wazazi wa mtoto paulina kwani aliharibika vibaya lakini mtoto peke yake ndio kichwa kilionekana.” amesema Kyando
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…