Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kiwanja hakina umiliki zaidi ya mtu mmoja
Kiwanja hakina mgogoro wa kisheria
Kiwanja hakiko kwenye hifadhi ya barabara au mazingira
Kiwanja kinafaa kwa ujenzi (Siyo tindiga, eneo la magadi, eneo la maporomoko ya ardhi au mkondo wa maji)
 
Uchaguzi duni wa ramani

Mara nyingi mtu humwita fundi na kumwambia kuwa “nataka unijengee nyumba ya vyumba vitatu”. Fundi anapouliza ramani yako iko wapi wao husema we angalia tu nzuri alimradi iwe ya vyumba vitatu. Hili ni kosa kubwa sana kwani husababisha watu wengi kujengewa nyumba ambazo hawazipendi.
 
Kutokufanya makadirio sahihi

Ni wazi kuwa umeona nyumba nyingi zikianzwa lakini hazimaliziki. Hili kwa kiasi kikubwa linatokana na kufanya makadirio na maandalizi duni kabla ya kuanza kujenga. Ujenzi wa nyumba unahitaji maandalizi mazuri hasa kifedha. Ni muhimu kujiandaa vyema kabla ya kuanza ujenzi ili usikwamie njiani.
 
Mambo unayoweza kufanya:

Weka makadirio ya gharama za ujenzi ili angalau uandae kiasi fulani cha pesa.
Nunua baadhi ya vifaa kabla. Unaweza kununua mchanga, mawe, kokoto, nondo, mabati n.k. Ili kupunguza matumizi ya pesa wakati wa ujenzi.
Weka mipango ya kutunza mahitaji yako mengine ya pesa kabla ya kuanza ujenzi. Kwa mfano ada za shule, kodi mbalimbali, chakula n.k.
Punguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kabla na wakati wa ujenzi. Ikumbukwe kuwa pesa nyingi zitahitajika kwenye ujenzi.
 
Kutokubainisha mahitaji

Mahitaji ya nyumba hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Hivyo ni vyema ukabainisha mahitaji yako kwa nyumba husika. Nimeshuhudia watu wakijenga nyumba na kuzivunja ua kuzifanyia marekebisho kila mwaka kutokana na kutobainisha mahitaji yao mapema.
 
Kurekebisha au kuvunja na kujenga upya nyumba yako kutakupotezea kiasi kikubwa sana cha pesa. Kwa mfano wengi hurekebisha nyumba zao ili kuongeza vitu kama vile jiko, choo na bafu, milango, madirisha n.k. ambavyo wangepanga mapema wangekuwa wameviweka mwanzoni.
 
Kutokuwaza mbeleni

Ni vyema kuwaza mbeleni kwani nyumba ni kitu utakachokitumia muda mrefu. Ni vyema ukafahamu vitu na mahitaji utakayoyataka kwenye nyumba yako kwa siku za mbeleni. Hili litakuwezesha kujenga nyumba utakayoitumia na kuifurahia kwa muda mrefu zaidi.
 
Back
Top Bottom