Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ni kweli mkuu baekje kuna kipindi walikinukisha vibaya sana eneo zima la three kingdom na walijenga diplomasia kubwa sana na nchi jirani hususan japan.
Baekje walikuwa na nguvu kubwa sana wakati wa utawala wa mfalme GEUNCHOGO ambaye alikuwa ni mfalme wa 13 wa taifa hilo na alikuwa ni mtoto wa 11 wa mfalme biryu.
baekje taifa lao kwa muda mrefu walijikuta wakigombeana madaraka kati ya koo mbili kubwa sana.
  • ukoo wa CHOGO ambao ndio anatokea mfalme geunchogo na ukoo wa GYE ambao alitokea mfalme gye.
  • baada ya kufa mfalme biryu nguvu ya utawala wa taifa hilo ulinyakuliwa na ukoo wa goi kuanzia mwaka 344-346 na ndipo geunchogo akafanikiwa kurudisha himaya ya utawala wa baekje kwenye koo ya CHOGO.
  • mfalme gye alikuwa ni mtoto wa kumi wa mfalme Bunseo ambaye mwaka 304 aliuliwa na ndipo biryu akashika madaraka kutoka ukoo wa chogo.kivyovyote utagundua ya kwamba koo hizi mbili zilikuwa ni mahasimu na kama tunavyofahamu kama ndugu wawili hamupatani basi anayefaidika na mgogoro ni adui, na adui mkubwa wa Baekje ni goguryeo ambaye aliutumia mgogoro wa koo hizi kwa ajili ya kunyakuwa maeneo ya BAEKJE.
  • ukisoma historia ya baekje utagundua ya kwamba wafalme 12 wa mwanzo 8 kati ya hao walitokea kwenye ukoo wa GOI na watano walitokea ukoo wa CHOGO.
  • aliposhika madaraka mfalme geunchogo ndio ilikuwa ni mwisho wa koo hizi mbili kupigana kwa ajili ya madaraka kwa sababu wafalme watano waliofuata wote walitokea ukoo wa CHOGO.
  • geunchogo alipoingia madarakani aliamua kupunguza nguvu kubwa iliokuwa ikishikiliwa na baadhi ya koo za kifalme (aristocracy) na pia kuanzisha mfumo wa local government kwa mara ya kwanza na pia alibadilisha makao makuu ya nchi na kuelekea hansan ambako kwa sasa ni kusini mashariki ya mji mkuu wa SEOUL.
  • kwenye kampeni yake ya kijeshi alifanikiwa kuiunganisha MAHAN,JEOLLADO, GAYA,NAKDONG RIVER yote yalikuwa chini ya himaya ya Baekje.
  • mwaka 371 alianzisha kampeni ya kuivamia goguryeo ambapo kampeni hiyo iliongozwa na mtoto wake mkubwa geungusu na kufanikiwa kuuteka mji mkuu wa pyongyang na pia kumuua mfalme gogugwon wa goguryeo.kwenye historia ya goguryeo ni mfalme mmoja tu ndiye aliyekufa vitani, hivyo basi goguryeo ikawa ni kama koloni la baekje.
  • pia alianzisha mfumo wa biashara kati ya baeje, china na japan na pia aliwapeleka baadhi ya wasomi nchini japan ili kueneza utamaduni wa baekje.
  • kwa hivyo kumbe gwanggaeto the great alikuwa ni mjukuu wa mfalme gogugwon ambaye aliuliwa na mtoto wa mfalme geunchogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…