Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3.Lee Bowyer- njano 100

Unaikumbuka ile Leeds United iliyokuwa moto uwanjani? Kipindi kile moja ya mastaa wake, alikuwa kiungo, Lee Bowyer. Alikuwa anapiga shoka huyo si mchezo. Lee Bowyer aliwahi kuzichezea West Ham United na Newcastle United. Soka lake la kibabe na kitendo cha kutokubali kushindwa kilimfanya staa huyo kuingia kwenye orodha ya wakali walionyeshwa kadi nyingi za njano kwenye historia ya Ligi Kuu England baada ya
 
3.Lee Bowyer- njano 100

Unaikumbuka ile Leeds United iliyokuwa moto uwanjani? Kipindi kile moja ya mastaa wake, alikuwa kiungo, Lee Bowyer. Alikuwa anapiga shoka huyo si mchezo. Lee Bowyer aliwahi kuzichezea West Ham United na Newcastle United. Soka lake la kibabe na kitendo cha kutokubali kushindwa kilimfanya staa huyo kuingia kwenye orodha ya wakali walionyeshwa kadi nyingi za njano kwenye historia ya Ligi Kuu England baada ya kulimwa kadi njano 100. Kwa sasa ni mstaafu.
 
2.Wayne Rooney- njano 101

Bora amekwenda kwenye Ligi Kuu Marekani maana jina lake lingechafuka zaidi kwa rekodi chafu kwenye Ligi Kuu England. Wayne Rooney ni mshambuliaji, lakini utashangaa amekuwa mmoja wa wachezaji wanaoongoza kwa kuonyeshwa kadi za njano kwenye Ligi Kuu England. Fowadi huyo anayeshikilia rekodi ya mabao Manchester United na England, ameonyeshwa kadi 101 katika historia yake ya kucheza kwenye ligi, huku akipita kwenye timu mbili tu, Man United na Everton. Rooney alizoa kadi akiwa Man United, na kumfanya ashike namba mbili kwa rekodi hiyo chafu.
 
1.Gareth Barry- njano 125

Gareth Barry ni kama vile hana alichobakiza kwenye soka kutokana na umri wake kuwa mkubwa. Lakini, kiungo wa West Brom, ataondoka kwenye Ligi Kuu England akiacha rekodi ngumu kuivunja. Ni rekodi ya kadi nyingi za njano baada ya kuonyeshwa mara 125 kwenye historia yake kwa mechi alizocheza kwenye EPL. Barry timu yake imeshuka na anaweza kuongeza rekodi hiyo kama ataamua kurudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…