Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Iko wazi kuwa, mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool Mohammed Salah ‘Mo’ yuko 'fiti' kushiriki michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Russia.

Taarifa kutoka nchini Misri zinasema kuwa matibabu ya kiungo mashambulizi huyo hayatachukua zaidi ya wiki tatu atakuwa amepona kabisa.
 
Hata hivyo, Mo Salaah ambaye yuko nchini Hispania kwa ajili ya matibabu ya bega hilo, timu yake itarusha 'kete' yake ya kwanza mapema Juni 15 itakapokipiga na Uruguay.

Mo Salah anayeshikiria rekodi ya kuifungia Liverpool mabao mengi, alipata maumivu hayo katika mchezo wao wa fainali wa Kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA) dhidi ya Real Madrid ambapo walimaliza kwa kufungwa mabao 3-1.
 
Ni katika harakati za kugombea mpira na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos jambo lililomfanya atoke uwanjani akitoa machozi ya uchungu kwa hofu ya kukosa fainali hizo zinazotarajia kuanza mwezi Juni nchini Russia.
 
ALAN Shearer anashikilia rekodi ya kuwa kinara wa mabao wa muda wote kwenye Ligi Kuu England baada ya kufunga mara 260 kwenye mechi za ligi hiyo. Straika huyo wa zamani wa Newcastle United na Blackburn Rovers anashikilia pia rekodi ya kupiga hat-trick nyingi baada ya kufanya hivyo mara 11, lakini anaongoza pia kwa penalti, akishikilia rekodi na penalti 58.
 
Rekodi hizo pengine zinasubiri kwa miaka mingi sana kabla ya kuvunjwa. Lakini, Ligi Kuu England ina rekodi zake nyingine, hazina mvuto, lakini ndiyo hivyo zimeshawekwa. Si rekodi za kujivunia, lakini ndiyo hivyo zimeingia kwenye vitamu vya kumbukumbu. Rekodi hizo ni za kuhusu kadi nyekundu na njano. Wakati ukijiuliza nani katisha kwenye rekodi hizo, hii hapa orodha ya wanasoka waliongoza kwa kadi nyingi za njano kwenye historia ya Ligi Kuu England.
 
6.Scott Parker- njano 92

Kuna wachezaji watano tu. Ndiyo, yani watano tu kwenye Ligi Kuu England ambao wameonyeshwa kadi nyingi za njano kuliko alizoonyeshwa kiungo, Scott Parker. Staa huyo wa zamani wa West Ham na Tottenham Hotspur, ameingie kwenye rekodi kwa kuonyeshwa kadi 92 za njano. Hata hivyo, kwa eneo lake la uwanja analocheza, idadi hiyo ya kadi imeonekana kuwa ya kawaida licha ya kuwapo na viungo wengine wa kati kama alivyokuwa Michael Carrick, alikuwa safi uwanjani.
 
5.Paul Scholes- njano 99

Rekodi yake ya kadi za njano kwenye Ligi Kuu England ndiyo kama zinavyosomeka hapo, ameonyeshwa njano mara 99. Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, huko ana kadi njano 32. Scholes katika kipindi chake cha uchezaji huko Manchester United alipendwa, aliogopwa na alichukiwa pia. Soka lake lilimfanya awe mwenye vitu hivyo vyote, lakini waliomchukia zaidi ni wapinzani wake wa ndani ya uwanja kwa sababu alikuwa hana breki, akija anakuja kweli kweli kwenye miguu yako.
 
4.Kevin Davies- njano 99

Utashangaa, Kevin Davies alikuwa mshambuliaji, lakini alikuwa anapiga mateke huyo si mchezo. Wakati anacheza kwenye kikosi cha Bolton na Preston, kiungo huyo wa ushambuliaji alifahamika vyema kutokana na ngwala zake alizokuwa akiwapiga wapinzani ndani ya uwanja. Jambo hilo limemfanya staa huyo kuingia kwenye orodha ya walionyeshwa kadi nyingi za njano kwenye historia yao ndani ya Ligi Kuu England baada ya kushuhudia akiingia kwenye kitabu cha waamuzi kutokana na kadi hizo mara 99. Kwa sasa ni mchambuzi.
 
Back
Top Bottom