Kwa wakati ule, Tutu aliyeonekana amekasirika sana aliwaambia viongozi wa ANC wakati wa mkutano wa waandishi wa habari “wajiangalie” na akawaonya dhidi ya kujisahau baada ya kushinda kila uchaguzi tangu mwaka 1994.
Katika kipindi hicho Jacob Zuma alikuwa rais wa ANC na nchi. Tutu, ambaye anatazamwa kama dira ya uadilifu kwa Afrika Kusini amekuwa akirudiarudia kuishutumu serikali ya ANC kwa kushindwa kuwasaidia raia wa Tibet ambao alisema “wamekuwa wakikandamizwa wazi na China” licha ya jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika Kusini kuushinda utawala wa kibaguzi.