Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika kampeni hii tumetenga lita 120,000 za maziwa zikiwa na thamani ya Sh60 milioni ili katika wiki hii ya unywaji wa maziwa kila mtoto apate,” anasema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mshikamano, Haiba Roy anasema kuna haja ya kuanzisha kampeni ya unywaji maziwa shuleni kila siku, ili kuwasaidia kiafya wanafunzi wengi wakiwamo wanaokwenda shule wakiwa hawajapata mlo wowote toka nyumbani kwao.
 
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mtwivilla, Florian Kilumile anasema uamuzi wa kampuni hiyo kufanya kampeni ya unywaji maziwa unapaswa kuungwa mkono na wadau wengine ikiwamo Serikali, ili kuwakumbusha wazazi kujenga utamaduni wa kununua maziwa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto.

Baadhi ya wanafunzi wanakiri kuwa wengi wao hawajawahi kunywa maziwa wakiwa nyumbani.
 
Nyumbani huwa sinywi maziwa kabisa kwa sababu wazazi hawaoni umuhimu huo ila wakielimishwa wanaweza kuanza kununua hata mara mbili kwa wiki,” anasema mwanafunzi Juma Salehe.

Salim Abri anasema inawezekana kila familia kutenga bajeti kidogo ili kuhakikisha inapata maziwa kutokana na umuhimu wake.
 
Sio tu kwa Iringa, zaidi ya watoto 2,000 wa shule za awali na msingi wenye umri wa hadi kufikia miaka tisa mkoani Njombe, wamenza kunufaika na mpango wa unywaji wa maziwa bure katika siku zote za shule kama mbinu ya kuimarisha afya na kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto.

Idadi hiyo ni miongoni mwa watoto 10,000 watakaofikiwa na programu hiyo katika mikoa ya Njombe, Iringa, Songwe na Mbeya wakati mradi huo unatekelezwa na shirika la kimataifa la Heifer kupitia moja ya miradi yake.
 
Meneja wa mradi wa uendelezaji wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD II) Tanzania, Mark Tsoxo anasema mpango wa unywaji maziwa shuleni unalenga kukuza utamaduni wa kunywa maziwa miongoni mwa watoto na kutengeneza mahitaji imara kwa ajili ya maziwa.

Katibu wa Tanzania Women Power (TPW), jijini Dar es Salaam Joyce Madenge ambaye pia ni mwalimu, anasema mpango wa maziwa shuleni unaweza kusaidia kujenga afya hasa za watoto wanaokosa fursa ya kuyapata.
 
Umuhimu wa maziwa mwilini

Mtaalamu wa Lishe kutoka Jukwaa la Lishe nchini (Panita), Debora Essau anasema umuhimu wa maziwa mwilini ni mkubwa hasa kutokana na virutubisho vilivyopo.

Anasema maziwa yanaweza kumfanya mtu kuwa na meno imara yanayong’aa, ngozi nyororo na ng’avu pia na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini.

Deborah anasema maziwa yana madini ya Calcium yenye kazi kubwa ya kujenga mifupa na meno.

“Kwa hiyo uimara wa meno na mifupa hutegemea pia unywaji wa maziwa, ni vizuri familia kujiwekea mkakati wa kila mtu kupata maziwa,” anasema.
 
Anasema maziwa pia yana vitamini ‘D’ kwa wingi ambayo inaweza kupatikana kwa kuota jua hasa wakati wa asubuhi.

Wataalamu wa afya wanasema upungufu wa vitamini hii unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya kuanzia udhaifu wa mifupa, matatizo ya nywele na hata udhaifu wa misuli.

Debora anasema mbali na vitamin hiyo, unywaji wa maziwa yana protini ambayo pia husaidia kujenga mwili.

“Kumbuka hiki ni kimiminika na kama unvyojua, unapokunywa kimiminika unalainisha choo hivyo unywaji wa maziwa unaweza kuufanya mwili kuwa na nguvu kwa kupata uhakika wa choo,” anasema.

Utafiti mmoja uliowahi kufanywa nchini Marekan ulieleza kuwa unywaji wa maziwa hasa yanayotokana na wanyama unaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.
 
Kwa mujibu wa utafiti huo vitamin D inayopatikana kwenye maziwa husaidia utengenezwaji wa kichocheo cha Serotonin kinachohusisha masuala ya ‘mood’.

Unaweza kupata hamu ya kula, kulala na wakati mwingine unywaji wa maziwa unaweza kupunguza uchovu na kumpa mtu raha.

Deborah anasema maziwa mazuri zaidi ni yale yatokanayo na wanyama kwani yana protini inayopatikana kwa kiwango cha hali ya juu.

“Maziwa pia hutupatia sukari japo kwa kiasi kidogo hivyo nisisitize tu kwamba ni muhimu kila mmoja kuzingatia unywaji wa maziwa katika milo ya kila siku,” anasema.
 
Kwa mujibu wa utafiti huo vitamin D inayopatikana kwenye maziwa husaidia utengenezwaji wa kichocheo cha Serotonin kinachohusisha masuala ya ‘mood’.

Unaweza kupata hamu ya kula, kulala na wakati mwingine unywaji wa maziwa unaweza kupunguza uchovu na kumpa mtu raha.

Deborah anasema maziwa mazuri zaidi ni yale yatokanayo na wanyama kwani yana protini inayopatikana kwa kiwango cha hali ya juu.

“Maziwa pia hutupatia sukari japo kwa kiasi kidogo hivyo nisisitize tu kwamba ni muhimu kila mmoja kuzingatia unywaji wa maziwa katika milo ya kila siku,” anasema.
 
Mtaalamu mwingine wa lishe Matrida Kassanga anasema unywaji huo wa maziwa haupaswi kupita kiasi.

“Kunywa maziwa kiwango kile kinachotakiwa mwilini, usinywe maziwa mengi hasa krimu kwa sababu unywaji huo unaweza kukusababisha uzito kupita kiasi,” anasema.

Salim Abri anasema kwa sababu maziwa hayawezi kudumu muda mrefu yasiposindikwa ipasavyo, kampuni hiyo itaanza matumizi ya teknolojia ya UHT kutengeneza aina mbalimbali za maziwa.

“Teknolojia hii ya Ultra High Temperature inawezesha maziwa yanayosindikwa kukaa kwa muda mrefu, hadi miezi sita bila kuharibika hata yakiwekwa katika maeneo yasio na mashine za kuyapooza,” alisema.

Anasema sio tu maziwa fresh hata yale ya mtindi yanazo faida nyingi kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.
 
Magari yaliotumika kwa zaidi ya miaka 15 hayatoruhusiwa nchini Uganda kuanzia Septemba mwaka huu kufuatia kuidhinishwa kwa marekebisho ya mswada wa trafiki na usalama barabarani mwaka 2018.
Watu wengi hununua magari makuu kuu kwasababu ya bei yake nafuu.
Serikali ya Uganda hatahivyo inataka kusitisha magari hayo kuingia nchini ikieleza kuwa sio salama kwa matumizi na huchafua mazingira.
 
Back
Top Bottom