Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakazi saba wa Mwanza na Shinyanga wamekamatwa na maofisa usalama katika kaunti ya Nzoia, mjini Kitale wakijihusisha na ombaomba na ulanguzi wa watu kinyume na sheria za Kenya.

Watu hao waliokamatwa jana na maofisa usalama ni Rhonda Makhenzi, Paolo Amos, Mikael Charles, Emmanuel Masudi, Mbekeso Masunga, Mecha Mabundu,na Pendo Njenzi.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Trans Nzoia, Samson Ole Kine amesema watu hao hawakuwa na nyaraka zinazowawezesha kuwa nchini humo na hawakueleza walichokuwa wakikifanya.

Amesema kabla hawajakamatwa, walikuwa wamejificha kwenye nyumba ya wageni na wengine wakiwa wamekodi vyumba katika mtaa wa Laini moja.
 
Amesema watuhumiwa hao walikuwa wanafanya kazi ya kuombaomba mitaani.

Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kuwa nchini Kenya kinyume na sheria ya nchi hiyo.

Watu wengine kutoka Tanzania walikamatwa mjini Eldoret wiki mbili zilizopita walipokuwa wakiomba pesa.

“Tuliambiwa watu wengi Eldoret ni matajiri na wakarimu zaidi kuliko watu wa kwetu,” amesema Maria Mapunda, mmoja wa watuhumiwa hao.
 
Jose anaonekana kuifahamu vizuri biashara hii ya kutumia walemavu kuomba fedha mitaani na ili aendelee kunisimulia nazidi kumdadisi na kumuacha ajiachie kujieleza.

“Kazi ya walemavu ni kula, kulala na kuvaa, basi. Pesa yote inachukuliwa na hao vijana wanaowasukuma ambao wakishapata wanawatumia mabosi mgao wao,” anasema Jose.
 
Huu ni mradi mzuri na biashara kubwa sana hapa mjini.”

Jose anasema kwa siku mlemavu mmoja huingiza kati ya Sh50,000 na 70,000 na ndani ya wiki anaingiza hadi Sh600,000.

“Ukishakusanya walemavu wako 10, unawatafutia baiskeli. Unaweza ukakodisha au ukanunua kwa kuwa kuna watu maalumu wa kukodisha baiskeli hizo na siku moja baiskeli moja inakodishwa kwa Sh4,000 na kwa wiki ni Sh25,000,” anasema.
 
Kwa mtu unayeanza biashara, unaweza kutumia baiskeli za kukodisha. Ukishapata baiskeli unatafuta vijana wako kumi ambao kazi yao ni kuwasukuma walemavu na kukusanyia pesa wanazopata walemavu hao kwa njia ya kuomba.”

Anasema ukimkabidhi kila kijana mlemavu mmoja, kazi yako inakuwa ni kukusanya fedha tu na unaweza kukubaliana nao kila mwezi ukawa unawataka hao vijana wakutumie Sh300,000 kwa mlemavu mmoja au kwa wiki wakutumie Sh100,000.
 
Anasema vijana wanaoishi kwake wana bosi wao mkoani Shinyanga ambaye kazi yake ni kukusanya walemavu kutoka vijijini na kuwapakiza kwenye basi na wakifika Dar es Salaam huwakodia vyumba kwenye nyumba za kulala wageni.

Akishafanya hivyo anachukua vijana pia kutoka vijijini na kuwapangia kwenye vyumba alivyowapangia walemavu wake na kumkabidhi kila kijana mlemavu mmoja. Baadaye huwatafutia baiskeli na kuingia mkataba nao wa malipo ya kila wiki au mwezi.
 
Kwa hiyo dada yangu kama una uwezo wa kuwashawishi watu namna hiyo na kuwaleta mjini, unaweza kuwa milionea kwa biashara hii tu,” anasema Jose.

“Dada yangu hii biashara inalipa sana lakini pia ukiifanya unatakiwa kuwa na usiri mkubwa na umakini wa hali ya juu. Si kazi ya kumhadithia kila mtu. Watanzania hatupendani, unaweza kujikuta unakamatwa kwani sheria za nchi zinakataza kuwachukua walemavu na kuwageuza mtaji wa kukuingizia fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…