Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya kumweleza Mama Pili kuwa tumemletea salamu kutoka kwa bintiye, alishikwa na mshangao na kuanza kujisemesha kwa lugha ya Kisukuma, akiuliza maswali mengi kuhusu maisha yake.

Anatuambia kuwa yeye ndiye mzazi wa Pili na kwamba jina jingine la binti huyo ni Doricas. Anasema jina lake ni Mery Mayonga na ana miaka 67.

“Eh! mwanagu jamani!” anasema kwa Kisukuma akionyesha kumkumbuka mtoto wake.
 
Hajawahi kuondoka hapa tangu nilipomzaa. Nimemkumbuka sana.” Wakati akisema hayo anainamisha kichwa chini kutafakari jambo na baada ya kuinuka anaanza kusimulia kwa hisia, akionekana kuwa na uchungu na mwanaye.

Anaeleza jinsi mtoto wake alivyochukuliwa na mtu aliyedai ni tajiri na kwamba alimuomba ili aende kufanya kazi ya kuomba mjini.

Baadaye anadadisi zaidi kuhusu maisha ya mwanaye ambaye ulemavu wake ni kichwa kikubwa.

“Sijui huko aliko anakula nini, analala wapi, anahudumiwa na nani,” anasema akionekana kujiuliza mwenyewe.
 
Nasikia kuna mvua kubwa inanyesha na mafuriko, sijui mwanangu kama yuko salama.”

Wakati wote huo alikuwa akizungumza kwa Kisukuma na mara nyingine alikuwa akisonya, kushika kidevu chake na paji la uso na kuinamia chini.

“Alikuja tajiri mmoja akasema anamtaka Dorcas aende naye mjini kufanya kazi ya kuomba hela kwa watu,” anaanza kusimuliwa kwa Kisukuma.

“Tajiri huyo anaitwa Mathias Nyanda Jihanga, lakini familia haimfahamu ni nani wala haina mahusiano yoyote naye.
 
Hatumjui. Alikuja tu hapa akasema anatafuta walemavu na kudai hiyo ndiyo kazi yake anakusanya walemavu na kuwapeleka mjini kuomba.

“Hatujui chochote akiwachukua anaenda kuwafanyia nini. Sisi alituambia kuwa atakuwa anatutumia pesa Sh150,000, tukamkubalia aende naye maana hali ya uchumi nyumbani ilikuwa mbaya.”

Anasema tajiri huyo ana ushawishi mkubwa na kwamba mbali ya fedha hizo, angekuwa anawatumia marupurupu mengi kama nguo, chakula na pesa.
 
Aliahidi kumnunua Pili nguo, kuwa anamlisha na kwamba atakuwa akiishi katika mazingira bora kwenye nyumba ya kupanga.

“Alisema kwenye hizo nyumba za kukodi kutakuwa na watu wa kumsaidia pale anapohitaji kuoga, hivyo hatapata shida yoyote,” anaeleza Mayonga.

Mazungumzo yetu na Mayonga yalikuwa yakizidi kunifungua akili kuhusu mradi huu wa kutumia walemavu kujitengenezea fedha.
 
Mazungumzo hayo yalizidi kunihakikishia kuwa ni kweli kuna watu wanatoka mjini na kuja kuwalaghai wazazi wa watoto walemavu kuhusu jinsi ya kuwatumia kutengeneza fedha, kuwaahidi malipo ya kila mwezi, matunzo mazuri na jinsi wazazi wanavyoridhia mradi huo na kuwaruhusu, na ukweli kwamba wazazi hawapati malipo hayo.

Lakini wakati wote tukizungumza na mama yake Pili akizungumza nasi, alikuwa amekataa simulizi yake kurekodiwa, akisema hadi mumewe arudi kutoka mjini alikokwenda kusikiliza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya kitongoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…