Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Figoni miongoni mwa viungo muhimu vya mwili wa binadamu. Kukosa kufanya kwake kazi kunaweza kusababisha magonjwa mazito na hata mauti. Figo limejengwa kwa viungo vingi na kazi zake ni nyingi.

Kazi zake mbili muhimu ni: kutoa uchafu unaoathiri mwili na wenye sumu na kuweko usawa wa maji (fluids), madini and kemikali.
 
Umbo la figo/structure
Figo hutoa mkojo kwa kutoa uchafu wenye sumu na maji zaidi kutoka mwilini. Mkojo unaotengenezwa katika figo hupitia kwenye mrija uitwao” ureta, na huteremka hadi kwenye kibofu (bladder) na mwisho hutoka kupitia mrija wa urethra.

Watu wengi (waume kwa wake) wana figo mbili.
Figo ziko sehemu ya juu na nyuma ya tumbo, pande zote za uti wa mgongo (tazama mchoro) zinakingwa zisiathiriwe na mbavu za chini.
Figo huwa ndani kabisa mwa tumbo kwa kawaida mtu hawezi kuzihisi.
Figo ni viungo jozi ya umbo la aragwe lenye urefu wa sentimita 10, upande wa sentimita 6 na wembamba wa sentimita 4. Uzito wake ni kati ya gramu 150 – 170.
Mkojo unaotengenezwa kwenye figo huteremka hadi kwenye kibofu kupitia kwenye ureta.
Ureta ina urefu wa karibu sentimita 25 umbo la mrija uliotengenezwa kwa misuli ya kipekee.
 
Kibofu ni kiungo chenye mwanya kilichoundwa kutokana na misuli inayolala.Kibofu kipo chini na mbele ya tumbo na ni stoo ya mkojo kwa muda. Chini na ndani mwa tumbo. Huwa kama mbwawa la mkojo.
Kibofu cha mtu mzima huweza kubeba 400 – 500 mililita ya mkojo na iwapo kimejaa karibu pomoni, mtu, hujisikia kwenda kukojoa.
Mkojo kwenye kibofu hutolewa kupitia urethra wakati wa kukojoa. Kwa wanawake, urethra yao ni fupi ilihali ni ndefu kwa wanaume.
 
Kwa nini figo ni muhimu kwa mwili?
Sisi hula vyakula vingi na tofauti kila siku.
Kiwango cha maji, chumvi na tindi kali (acids) katika miili yetu hutofautiana.
Ile hali inayoendelea ya kubadilisha chakula ili kilete nguvu hutoa vitu/sumu mwilini.
 
Vitu hivi husababisha utofauti wa kiwango c tindi kali (acids) mwilini. Huu mkusanyi isiyohitajika huweza kuhatarisha maisha.
Figo hubeba kazi muhimu sana ya kusafish vyenye sumu, tindi kali(acid) ya sumu na vi materials) hufanya hivyo wakati huo huo i kuhakikisha usawa wa kiwango cha maji, el cha tindi kali (acid base).
Kazi za figo ni zipi?
Kazimuhimu ya figo ni kutengeneza mkojo na huondoa vitu visivyofaa, chumvi chumvi ya ziad mwilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…