Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
 
 
 
SUBIRI. Unaongea na mimi au unaongea na simu? Jamani, mmemsikia Cristiano Ronaldo huko? Ni hivi, anachosema ni kwamba anataka alipwe Pauni 1.35 milioni kwa wiki ili asaini dili jipya Real Madrid.

Hicho ndicho kinachosemwa, kwamba Ronaldo amewaambia Real Madrid wampe mshahara wa Pauni 1.35 milioni kwa wiki ili abaki kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Santiago Bernabeu. Hivyo ndivyo inavyoelezwa kwa taarifa za kutoka Hispania.
 
Hatima ya staa huyo mshindi wa mara tano wa Tuzo ya Ballon d’Or, imekuwa kwenye utata mkubwa baada ya hivi karibuni kudai anafikiria kuachana na timu hiyo mara tu baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na Ronaldo aliacha kufurahia ushindi dhidi ya Liverpool na kuanza kuzungumza kwamba ataondoka.
 
Akwendreeee
 
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, amesema Ronaldo hawezi kuondoka kwenye klabu hiyo na mambo kama hayo yamekuwa yakizungumzwa kila wakati kinapofika kipindi cha uhamisho wa wachezaji huko Ulaya.

Ripoti zaidi zinadai Ronaldo anajaribu kutikisa kiberiti huko Real Madrid kwa maana kwamba hafurahii mshahara wake anaolipwa sasa ambao unamfanya afunikwe na mastaa wenzake, Lionel Messi wa Barcelona na Neymar wa PSG.
 
El Confidencial linaripoti kwamba wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes, amesema mkataba mpya anaotaka mteja wake alipwe unapaswa kuwa wenye thamani ya Pauni 70 milioni kwa mwaka kabla ya makato ya kodi.

Suala lililopo ni kama Real Madrid itakubaliana na hilo, jambo ambalo litamfanya Ronaldo awe anaweka mfukoni Pauni 44 milioni kila baada ya miezi 12, ikiwa ni sawa na Pauni 841,000 kwa wiki — kwa dili la miaka mitatu itawagharimu wababe hao wa Bernabeu kiasi cha Pauni 210 milioni.
 
Hata hivyo, ripoti nyingine zimebainisha Los Blancos hawafikirii kukubaliana na matakwa hayo, hasa ikizingatiwa mchezaji mwenyewe wakati mkataba wake huu utakapofika mwisho, atakuwa ametimiza umri wa miaka 36, ambao utakuwa mwisho wa maisha yake kisoka.
 
Wamtoe haraka aende uarabuni
 
Ronaldo anachotaka ni kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi ya Messi na Neymar. Dili lake la sasa linamshuhudia Ronaldo akilipwa Pauni 350,000 kwa wiki, wakati Neymar analipwa Pauni 619,000 kwa wiki na Messi analipwa Pauni 673,000 kwa wiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…