Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MSHINDI
*****************
Mshindi
Nkamiji
Nkindi
Nyasinde
Omusingi
Umushindi
Untoli

Wewe ni jemedari mshindi
Ushindaye mioyo
Iliyopondwa pondwa na dunia
Mioyo migumu iliyokakawana
Kama ngozi ngumu ya ngao ya Goliati
Katika bonde la vita vya kukata maneno.

Waja kimya kimya na manati yako
Iliyopakwa asali mpya tamu tononofu
Katika midomo yako mizuri itemayo baraka

Napenda ulivyozipukutisha hisia zangu kinzani
Na kunionyesha amani ya ajabu kondeni
Tulikopanda maua yetu waridi yasiyonyauka.

Wewe ni Mshindi
Wewe ni Nkamiji
Wewe ni Nkindi
Wewe ni Nyasinde
Wewe ni Omusingi
Wewe ni Umushindi
Wewe ni Untoli

KAMWE USIBADILIKE

By SYB (JF)
3/6/2018
 
View attachment 793513
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom